ILIPOISHIA
“Nafanya hii, kwa ajili yakulipiza kisasi cha mume wangu”
“Ngoja kwanza, nipo tayari kufa, ila ninakuomba usimuue mke wangu”
Nilizungumza kwa ujasiri, nikiwa nipo tayari kwa kufa, Madam Mery
akalinyanyua panga lake juu, akalishusha kwa kasi kwenye mkono wangu wa
kulia
ENDELEA
Nikatoa ukulele mkali, ulio mfanya madam Mery kusitisha zoezi lake
kuukata mkono wangu, panga lake likiwa limesimama sentimita chache
kutoka ulipo mkono wangu
“Madam, ninakuomba unisamee”
Nilizungumza huku machozi yakiendelea kunimwagika usoni mwangu, madam Mery akanitazama kwa macho ya hasira yaliyo jaa
ukatili mkubwa, akawatazama Victoria na John ambao macho yao yote yalikuwa kwetu
“Natambua kwamba mimi nimkosaji sana kwako, ninastahili kufa mbele yako,
ila si mbele ya macho ya mke wangu.Mtazame jinsi alivyo katika hali
yake.Mule ndani amebeba kiumbe kama ulicho kuwa umekibeba wewe, miezi
tisa, na Derick akakiangamiza mbele yetu.Yule ni mwanamke mwenzako
ambaye anauchungu kama wewe”
Nilizungumza huku machozi yakiendelea kunimwagilka usoni mwangu, madam
Mery kwa mbali machozi yakaanza kumlenga lenga, macho yake yamebadilika
rangi na kuwa mekundu kiasi huku sura yake ikiwa imejaa mikunjo kwenye
paji lake la uso akinitazama kwa uchungu sana
“Mery mimi pia ni binadamu, kumbuka ni mambo mangapi tuliyafanya tukiwa
pamoja, vuta kumbukumbu ni vitu vingapi tulishiriki tukiwa pamoja,
Eheeee, leo hii unataka kuimwaga damu yangu, leo hii unataka kunisulubu
kikatili, le……..”
“Eddy STOP TALKING”(Eddy nyamazakuzungumza)
Madam Merry alizungumza kwa sauti ya juu, yenye uchungu ndani
yake.Akalitupa chini panga lake alilokuwa amelishika.Machozi mengi
yakaanza kumbubujika usoni mwake, John na Vivtoria wakabaki wakimtazama
madam Mery, ambaye taratibu alianza kupiga hatua za kuelekea kwenye gari
lake alilo kuja nalo
“Madam Vipi?”
John alizungumza huku akimwafwata madam Mery kwa nyuma
“John ninakuomba uniache”
Madam Mery aluzungumza huku akiunyanyua mkono wake mmoja akimzuia John asimfwae anapo elekea
“Ila madam haya sio makubaliano yetu”
“John sipo sawa nimekuambia usinifwate”
Madam Mery alizungumza kwa sauti ya ukali, huku machozi yakiendelea kumchuruzika usoni mwake.
“Sasa Madam tumfanye nini Eddy?”
Madam Mery akageuka kwa hasira, hadi John akastuka kidogo, akanitazama
jinsi machozi yanavyo nimwagika, akayafumba macho yake kwa sekunde
kadhaa, akionekana akifikiria kitu cha kufanya juu yangu.
“Kesho nimkute akiwa hai”
Madam Mery alizungumza kwa sauti ya upole, kisha akaelekea lilipo gari
lake, akafunguliwa mlango na mlinzi wake, akaingia ndani ya gari na
wakaondoka zao.John akalisindikiza magari ya Madam Merry yanayotoka
kwenye geti kubwa la Godauni, lilipo fungwa taratibu John akanigeukia,
akanitazama kwa macho ya dharau huku Victoria akiwa amejichokea, kwani
ninaamini mipango yao waliyo kuwa wameipanga dhidi yangu
imeharibika.John akamfwata Victoria sehemu alipo simama,
wakanong’onezana kwa muda kasha wakamtama Phidaya ambaye muda wote,
amejilaza chini huku machozi yakimwagika kwa uchungu.
“Mchukueni huyo Malaya mumrudishe mulipo mtoa”
John aliwaamrisha watu wake, wakamnyanyua Phidaya na kumbeba juu juu,
japo anajitahidi kujitoa mikononi mwa watu walio mbeba, huku aikiliita
jina langu kwa sauyti ya juu, ila hakuifanikiwa kujitoa mikononi mwao
John akapiga hatua hadi katika sehemu nilipo fungwa, akanitazama kwa
muda, huku macho yake yakiwa yamejaa dharau kubwa, akanitemea mate ya
usoni, akiyasindikiza kwa kofi zito lililo tua kwenye shavu langu la
kushoto
“Mmmmmm Eddy, unajisikiaje?”
John alizungumza huku akivifikisha viganja vyake, na kuvipuliza taratibu
taratibu.Akanishika sikio langu la upande wakulia, akaanza kulivuta kwa
nguvu zake zote, nikaendelea kuugulia maumivu ndani kwa ndani, sikutoa
sauti yoyote kwenye kinjwa changu
“Waooo, unajifanya komandoo usikii maumivu eheeee?”
John alizungumza, huku akiliachia sikio langu.Akaanza kunitandika vibao
mfululizo kwenye mashavu yangu, hasira ikazidi kumiliki nafisi yangu.
“John, tumpeleke kisimani, hapo unajisumbua bure”
Victori alitoa wazo ambalo John alilikubali, wafanyakazi wao
wakanishusha kwenye meza, majamaa wawili wakanibeba kwenye mabega yao.
kama wawindaji walio beba swala waliye muua kwenye mawindo yao.Tukaingia
kwenye moja ya ukumbi mkubwa wenye mwanga hafifu, unao pita kwa kutumia
madirisha machache yaliyopo juu yake.Wakanibwaga chini, na kunifanya
nitoe mguno wa maumivu kutokana na kujiumiza sehemu ya paja langu,
nililo pigwa risasi Taa kubwa zenye rangi nyeupe zikawaka na kulifanya
eneo zima la ikumbu kuponekana vizuri, kuna mashimo makubwa mawili, kwa
haraka nikatabua ndio hivyo visima wanavyo vizungumzia, mabaunsa walio
kuwa wamenibeba, wakaufunga mwili wangu kwa kamba ngumu aina ya manila.
“Eddy utakufa kifo kibaya sana”
John alizungumza huku akiwa ameniinamia
“Usiombe nikatoka, kwenye mikono yeno, utajuta”
Nilizungumza kwa kujiamini sana, John akaanza kucheka kwa dharau, huku akinipiga piga mashavuni mwangu
“Eddy huwezi kutoka mikononi mwangu, nakujua wewe vizuri sana.Huwezi fanya chochote dhidi yangu.Muda wako umekwisha kaka”
“Angalia wakwako ndio utakuwa umekwisha”
John akaanza kunipiga mateke mfululizo kwenye mbavu zangu, nikaendelea
kutoa sauti ya maumivu ila John hakunionea huruma zaidi ya kuendelea
kunipiga kwa nguvu zake zote
“Mchukueni na mukamdumbukize kwenye kisima”
John aliwaamrisha watu wake, wakanibeba, kabla hawajaondoka na mimi, Victoria akawazuia.Akapi ga hatua hadi sehemu tulipo simama
“Eddy nakupenda kaka yangu, kwaheri”
Victoria alizungumza huku akinibusu shavuni mwangu, akawarusuhu watu
kuonipeleka kwenye kisima kilichopo kwenye huu ukumbi, kwa jinsi walivyo
nifunga kamba mwili wangu sikuweza kufanya kitu cha aina yoyote zaidia
ya mwili wangu kunyooka moja kwa moja, mithili ya mtu aliye fariki
dunia.Wakanifunga kwenye kamba nene, tartibu wakaanza kunishusha kwenda
chini, taratibu.Giza jingi lililo tawala ndani ya shimo hili, likazidi
kuniogopesha na kunifanya nizidi kuchanganyikiwa.Nikastuykia nikigusa
chini, kwenye shimo hili lenye futi zaida kumi na mbili. Gafla nikaanza
kuhisi vitu vidogo vidogo vikinitambalia mwilini mwangu, nikastukia
mwili wangu ukianza kupata maumivu maklali yaliyo tokana kung’atwa na
wadudu wadogo ambao sikujua ni waduudu wa aina gani, jambo lililo
nifanya nitoe ukelele mkali sana
ITAENDELEA
ENDELEA KUDWATILIA SIMULIZI HII, KUPITIA WHATSAPP KWA MALIPO YA SH. 3000 TU KWA MWEZI, NO 0657072588,
NITAKUTUMIA INBOX BAADA YA MALIPO, KAMA ULILIPA PESA YAKO NA HUKUPATA
HUDUMA KWA SABABU ZILIZOPO NJE YA UWEZO WANGU, NITEXT INBOX WHATSAPP,
FACEBOOK NAWE NITAKUHUDUMIA.ASANTE
****SORRY MADAM****(72)
WRITTER……………………………………….EDDAZARIA
G.MSULWA
www.storyzaeddy.com
ILIPOISHIA
Giza jingi lililo tawala ndani ya shimo hili, likazidi kuniogopesha na
kunifanya nizidi kuchanganyikiwa. Nikastuykia nikigusa chini, kwenye
shimo hili lenye futi zaida kumi na mbili. Gafla nikaanza kuhisi vitu
vidogo vidogo vikinitambalia mwilini mwangu, nikastukia mwili wangu
ukianza kupata maumivu maklali yaliyo tokana kung’atwa na wadudu wadogo
ambao sikujua ni wadudu wa aina gani, jambo lililo nifanya nitoe ukelele
mkali sana
ENDELEA
Wadudu wenye meno makali, wakazidi kuushambulia mwili wangu jambo lililo
nifanya nizidi kuchanganyikiwa na kuanza kukiona kifo kikisimama mbele
yangu, nilicho kuwa nikikisubiria ni pumzi yangu kukatika name niesabike
kama mfu kati ya mamilioni ya watu walio tangulia mbele za haki, masaa
kadri yalivyo zidi kukatika ndivyo jinsi nilivyo zidi kupata maumivu
makali yasiyo mna kikomo, ikafikia kipindi kelele na maumivu yangu
hayakupata msaada wa aina yoyote kutokwa kwa mtu yoyote
“Eheee Mungu ninakuomba unisaidie”
Niliamua kumkumbuka Mungu wangu, kama kuna uwezo wowote ambao anaweza
kunipatia, kwa wakatui huu, sikua na ubishi wa aiana yoyote kwani ndio
tayari nipo kwenye shimo la kifo.Giza likaanza kutoweka taratibu na
mwanga mkali wa jua ukitokea juu ya paa lililo funguliwa muda mchache
uliopita ikiashiria kwamba asubuhi nma mapema kumepambazuka, hapa ndipo
nikagundua aina ya wadudu wanao nishambulia kwamba ni ng’ee wadogo
wadogo wenye meno kali sana.Nguvu za mwili wangu zikaanza kuniishia
kadri ya muda unavyo katika, mwili mzima wote umevimba kwa maumivu
makali niliyo yapata. Nikaanza kuzisikia kelele za watu wakizungumza
ndani ya ukumbi huu, huku kutikana na umbali niliopo kwenda chini kwenye
kwenye shimo sikuelewa ni mazungumzo ya aina gani ambayo
wanayanzungumza, taratibu nikaaza kuvutwa kwenda juu, na nikatolewa
ndani ya shimo na watu walio niiingiza ndani jana.
“Duu huyu jamaa ana roho yap aka, bado yupo hai”
Jamaa mmoja alizungumza huku akinitazama na kunigeuza geuza kwa mguu
wake alio valia kiatu kigumu sana, na kila alipokua akinmigusa katika
mwili wangu, kwangu ilikuwa ni maumumi makali yasiyo elezeka
“Si bora tumuue tuu”
“Tukimuua unadhani bosi atatuelewa?”
“Sasa mtu ameumuka kiasi hichi unadhani
kwamba atapona huyu?”
“Sina uhakika ila tusubiri hao mabosi wetu wakija
watoe uamuzi juu ya hili”
Jamaa waliendelea kushauriana huku wakiwa wamenizunguka, katika sehemu
waliyo nilaza huku kamba waliyo izungusha mwilini mwangu ikiendelea
kubaki kama walivyo nifunga, jamaa mmoja ajachukua ndoo ya maoja na
kutoka nje, wakabaki jamaa watatu wakiwa wamenizunguka. Huku wakiwa
wanavuta sigara zao.Jamaa aliye toka na ndoo akarudi na kuisimamisha
pembeni
yangu
“Umeweka nini humo?”
“Kuna maji ya yabaridi nahitaji kumuogesha huyu mwehu”
Jamaa pasipo kufikiria mara mbili ni maumivu ya aiana gani nitayapata,
akaanza kunimwagia kuanzia juu hadi chini huku akiungana na wezake
katika kunimwagia maji hayo, yaliyo zidi kuviumiza vidonda vyangu.
“Cheki jinsi anavyo babaika”
Mmoja alizungumza huku akininyooshea kidole, wakinicheka jinsi ninavyo
garagara chini na kulia kwa maumivu makali ninayo yapata mwilini mwangu
“Bosi anasema mumtoe, mumpeleke kule kwenye godauni”
Jamaa mmoja aliye ingia muda si mrefu aliwapa wezake ujumbe walio anza
kuutekeleza ndani ya dakika moja mbeleni, nilidhani watanibeba kama
walivyo fanya jana walipokua wakiniingiza ndani ya ukumbi huu. Wakaanza
kuniburuta huku wakiwa wanaivuta kamba waliyo nifunga nayo.Tukafika
kwenye godauni la jana, nikamkuta John akiwa na Victoria wamesimama
wakitungojea tutokee katika sehemu tuliyo simama
“Habari za asubuhi Mr Eddy”
John alizungumza huku akinizunguka zunguka katika sehemu niliyo lazwa,
hata kinywa changu hakikuwa na nguvu ya kufunguka kutokana na maumimu
makali niliyo yapata kutoka kwa wadudu walio nishambulia usiku mzima
“Ninaimani leo inakuwa ni siku ngumu sana kwako”
John aliendelea kuzungumza huku akiwa amesimama pembeni yangu
akinitazama chini, sukuamini Yule John niliye kua nikimsaidia mambo
mengi kipindi tunasoma leo hii ndio mtu anaye nifaniyia ukatili wa aina
hii
“Mtoeni Yule Malaya”
Walinzi wao wakatii agizo walilo ambiwa na mkuu wao ambaye ni John,
ndani ya dakika kadhaa wakarudi wakia wameongozana na mke wangu Phidaya,
ambaye amechakaa kwa kiasi kikubwa huku nywele zake zikiwa zimechanguka
kama mwenda wazimu, uzuri wake wote umepotea kwenye sura yake, sura
yake imejaa alama nyingi za vidole ikishiria kwamba kuna mtu au watu
walimpiga muda mchache ulio pita
“Eddy ninakumbuka kipindi tunasoma kombi ya
PCB, ulikua unapenda sana kuwapasua vyura kuona ni kitu gani kipo ndani
ya matumbo yao, sasa leo na mimi ninahitaji kumpasua mke wako nione ni
kitu gani ambacho amekibeba ndani ya tumbo lake hadi likawa kubwa kiasi
hichi” John alizungumza huku akianza kuvaa gloves nyeupe, macho yangu
yakakutana na macho ya Phidaya ambaye muda wote anabubujikwa na machozi
mengi usoni mwake, akaanza kutingisha kichwa pasipo kutambua ni nini
maana ya yeye kukitingisha kichwa chake
“Ohhh naona wifi anahuzuni sana, ila John nimepata wazo”
Victoria alizunguimza huku akimtazama John anaye chagua chagua kisu
kikali kwenye moja ya meza fupi iliyomo ndani ya godauni hili
“Wazo gani mke wangu”
“Mimi ninaona tumpe uchaguzi wifi yangu kipenzi”
“Ehee endelea mama”
“Mimi ninaona achague kati ya haya mambo mawili, kumfanyia upasuaji na
ukitoe hicho kiumbe cheke au amuue mume wake kwa mikono yake yeye
mwenyewe”
Nikamuona jinsi Phidaya alivyo stuka na kuzidi kumwagikwa na machozi
mengi usoni mwake, nikamtazama Phidaya ambaye amechanganyikiwa kwa mambo
aliyo ambiwa na Vicvtoria
“Yeee hilo ni wazo zuri mpenzi, yaap Shemeji, uamuzi upo mikononi mwako,
una dakika mbili za kujifikiria, wewe kuondoka duniani, au wewe
kumuondoa mume wako duni ani”
John akaivua saa yake ya mkononi na kumkabidhi Phidaya, akimuomba afanye
kama alivyo agizwa.Phidaya akanitazama mimi kwa macho yaliyo jaa
uchungu kisha akamtazama John anaye piga mluzi, ulio jaa dharau.
“Dakika zinakwisha shemeji”
Phidaya akajiinamia chini, kisha akanyanyanyua kichwa achake na
kunitazama tena kwa mara nyingine pasipo kuzungumza kitu cha aina
yoyote.Akamrudishia John saa yake kisha, akanyoosha mkono wake kwa John
akiashiria kwamba kuna kitu anakiomba
“Nini?”
John alimuuliza Phidaya aliye baki amemnyooshea mkono mmoja pasipo kusema kitu cha aina yoyote
“Kisu”
John akatabasamu na kuchagua kisu kikubwa kiasi chenye ncha kali na
kinacho ng’aa, akamkabidhi Phidaya, aliye kishika vizuri na kuanza
kupigha hatua hadi sehemu niliyo lala, macho yangu yakanitoka kwani
sikuelewa Phidaya anataka
kufanya kitu cha aina gani
“Eddy ninakuomba unisamehe, nafanya hivi kwa ajili ya mwanangu aliye
tumboni mwangu, ninaimani nizawadi tosha uliyo nipatia mimi”
Phidaya alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake na kunitazama kwa macho makali.Machozi yakaanza kunimwagika taratibu
“Phi…d….”
“Shemeji usimsikilize huyo muue”
John alizungumza kwa sauti kali, iliyo zidi kumtetemesha Phidaya aliye changanganyikiwa
“Usipo muua ninakufumua tumbo lako hilo, kubwa hilo sasa upo tayari kupoteza maisha yako na
mwanao?”
John aliendelea kuzungumza kwa sauti ya ukali na yajuu kiasi
“Hembu jitazame wewe mwenyewe, jinsi ulivyo mzuri, mwanamke mwenye
kupendeza, hadi sasa hivi sijatambua ni kwanini unapata tabu kwa ajili
ya mpumbavu mmoja, ambaye sijuu mumekutana wapi?”
John aliendelea kumshawishi Phidaya kufanya anacho hisi kwao kitakuwa ni furaha
“Wifi, mbona wanaume wapo wengi tuu, utapata wanaume wazuri zaidi ya
huyo mume wako, huu ni wakati wako sasa, uhai wako upo juu ya mikono
yako”
Victoria naye aliamua kusema kitu juu ya Phidaya aliye anza
kuchanganyikiwa na kujikuta akiwa amekishika kisu kwa mkono mmoja,
taratibu Phidaya akaikutanisha mikono yake kwa pamoja katika kishikizo
cha kisu, taratibu akaanza kuinyanyua juu akijiandaa kikishusha kwenye
mwili wangu na wala sikujua ni wapi kitwakwenda kutua
“I say kill him”
John aliendelea kuzungumza kwa kufoka huku akimtazama Phidaya anaye
mwagikwa na jasho mwili mzima, sikuwa na uwezo wa kufanya kitu cha aina
yoyote kutokana mwili wangu wote imefungwa kwa kamba
“Eddy am sorry”
Phidaya akakishusha kisu kwa nguvu, kabla hakijatua kwenye kifua changu
akakisimamisha na kukitupa pembeni na kuniangukia kifuani mwangu na
kunikumbatia huku akilia kwa sauti ya uchungu
“Nakupenda mume wangu, wewe ni baba wa wanangu, siwezi kukuua kwani sijui nitamjibu nini
mwanangu pale atakapo uliza yupo wapi baba”
Phidaya alizungumza huku akiendelea kunikumbatia kifuani mwangu, machozi yakeendelea kunimwagika huku nikimtazama
Phidaya, Phidaya akasimama kwa hasira na kumtazama John
“Kama unataka kuniua niue tu, ila siwezi kumuua mwanaume wa maisha
yangu, niliye jiapiza kwamba sinto weza kumuacha katika maisha yangu
yote hadi ninaingia kaburini”
Phidaya alizidi kuzungumza kwa hasira huku akiwa amelishika tumbo lake
kwa mkono wa kulia, akichechemea na kumfwata John aliye pigwa na butwaa
“Ni mangapi aliyo kusaidia rafiki yako Eddy, ni vitu vingapi alivyo
kutendea Eddy, leo hii unataka kumuangamiza mbele yako, unataka
kupelekeshwa na huyo mzungu wako.Kumbuka huyo sio muafrika mwenzio,
kumbuka huyo ndio aliye kunyanyasia wazazi wako.Leo hii bado unaende………”
Victori akapimtandika Phidaya kibao kilicho muangusha chini, ila Phidaya
akanyanyuka na kusimama, huku akiyumba yumba mithili ya mlevi.Gafla
nikaanza kuona maji maji mengi yakichuruzika kwenye miguu ya Phidaya,
ambaye alianza kulishika tumbo lake, huku akilia kwa uchungu mkali
sana.Nikaanza kujibiringisha taratibu nikilisogelea eneo alilo lala
Phidaya huku akiendelea kulia kwa uchungu
“Eddy……”
Phidaya aliita huku akilia kwa uchungu, miguu yake akiwa aimeipanua, jasho jingi likianza kumwagika
“Ba……by p..usssh”
Nilizungumza kwa kujikaza huku nikiwa sina msaada wowote kwa mke wangu,
John na watu wake wakabaki wakiwa wametukodolea mimacho huku wengine
wakicheka kwa dharau, Victoria akataka kuja sehemu tuliyopo mimi na
Phidaya ila John akamzuia, huku akimshika mkono.
“Acha tuone watafanyaje”
John alizumngumza kwa dharau
“Push baby”
Nilizungumza huku machozi yakiendelea kunimwagika usini mwangu Phidaya
akazidi kujikakamua, huku akiendelea kulia, kutokana Phidaya ni nesi
kidogo kuna mbinu za uzalishaji aliana kuzitumia kwani hapakuwa na
msaada wowote kwake zaidi ya mimi kumchochea kwa maneno aweze kumsukuma
mtoto atoke nje
“Anakuja baby anakuja”
Phidaya alizungumza kwa uchungu huku akiendelea kuzidi kujikakamua
kumzaa mtoto wetu, wazo likanijia haraka, japo ninamaumivu makali mwili
mwangu ila nikajigeuza haraka na kuiweka miguyu yangu karibu na miguu,
ya Phidaya aliye
zidi kujikaza katika kumleta kiumbe change duniani. Nikamshuhudia
mwanangu akitoka taratibu na kufikizia kwenye miguu yangu, Phidaya
akajitahidi hadi mtoto wangu wa kiume akalala kwenye miguu yangu, iliyo
fungwa kamba kwa pamoja
“Duuuu hongereni sana”
John alizungumza huku akiichomoa bastola yake kiunoni
“John unataka kufanya nini?”
Victori alizungumza, huku akimtazama John aliye anza kuifunga bastola yake kiwambo cha kuzuia sauti
“Sifanyi chochote mke wangu”
John akanisogelea hadi sehemu tuliyo jilaza, akanitazama kwa muda, mimi pamoja na mwanangu aliye anza kulia
“Mwanao ni mzuri sana”
John alizungumza huku akimtazama mwanangu pamoja na mama yake aliye jilaza, akiwa ameishiwa nguvu za mwilini mwake
“Goodbye my friend”(Kwaheri rafiki yangu)
John alizungumza kwa sauti ya upole nikastukia risasi kadha zikitua
kifuani mwangu na kuninyamazisha kimya katika sehemu niliyo lala
ITAENDELEA
ENDELEA KUDWATILIA SIMULIZI HII, KUPITIA WHATSAPP KWA MALIPO YA SH. 3000 TU KWA MWEZI, NO 0657072588,
NITAKUTUMIA INBOX BAADA YA MALIPO, KAMA ULILIPA PESA YAKO NA HUKUPATA
HUDUMA KWA SABABU ZILIZOPO NJE YA UWEZO WANGU, NITEXT INBOX WHATSAPP,
FACEBOOK NAWE NITAKUHUDUMIA.ASANTE
SORRY MADAM 73
WRITTER……………………………………….EDDAZARIA
G.MSULWA
www.storyzaeddy.blog.com
ILIPOISHIA
John akanisogelea hadi sehemu tuliyo jilaza, akanitazama kwa muda, mimi pamoja na mwanangu aliye anza kulia
“Mwanao ni mzuri sana”
John alizungumza huku akimtazama mwanangu pamoja na mama yake aliye jilaza, akiwa ameishiwa nguvu za mwilini mwake
“Goodbye my friend”(Kwaheri rafiki yangu)
John alizungumza kwa sauti ya upole nikastukia risasi kadha zikitua
kifuani mwangu na kuninyamazisha kimya katika sehemu niliyo lala
ENDELEA
***
Sauti ya milio ya ndege nikaanza kuisikia kwa mbali kwenye masikio
yangu, taratibu nikajaribu kuyafumbua macho yangu kuweza kuona n kitu
gani kinacho endelea ila, ukungu mwingi umawa umetawala kwenye mboni
yamacho yangu, jamvo lililo nifanya nisione kitu cha aina yoyote,
nikajaribu kupapasa katika sehemu niliyo lala, nikagundua kwamba
nimelalia kitanda cha kamba, ila sikuweza kutambua ni sehemu gani
niliyopo.Muda jinsi ulivyo yoyoma ndivyo nilivyo weza kugundua kwamba
eneo nililopo, kuna watu wanao zungumza lugha nisiyo ijua
"Nipo wapi?"
Nilijarivu kuzungumza huku nikijitahidi kunyanyuka kutoka katika kitanda
nilicho lala ila milono ya watu si chini ya wanne wakanirudusha kulala
tena kwebye kitanda.Sauti za wanaume pamoja na wanawake zikaendelea
kupenya kwenye masikio yangu, nilipo anza kusikia milio ya watoto wadogo
wakicheza na wengine kulia ndipo nilipo amini kwamba eneo hili ni
salama kwa maisha yangu
Nikawasikia wakiendelea kunong'oneza, mara sauti ya kike ikasikika,
ambayo sikuweza kuisikia tangu wàlipo anza kuzungumza watu hawa, ambao
hadi sasa hivi siwezi kuwaona vizuri zaidi ya vivuli vyenye giza,
vilivyo simana pembeni ya kitanda nilicho kilalia.Nkasikia
wakiyazungumza maneno niliyo yasema dakila kadhaa za nyuma nikiwauliza
kwamba hapa nilipo ni wapi
"Hei"
Sauti ya msichana hiyo ilinisemesha, ila sikujua anataka kusema kitu gani
"Nipo wapi, dada?"
Nliyarudia maneno yangu niliyo yazungumza hapo awali
"Unazungumza kiswahili wewe?"
Msichslana huyo aliniuliza, kwa lugha ya kiswahili jamvo lililo nifanya
nizidi kufarijika moyoni mwangu na kuamini kwamva nimepata mwokozi
katika wakahi huu mgunu nilio nao katika yangu maisha
"Ndio, ndio dada"
Niliitikia kwa haraka ila hata ninaye zungumza naye asibadili mawazo ya kunisaidia mimi
"Unaitwa nani?"
"Eddy, Eddy dada yangu"
Nikamsikia msichana huyo akizungumza na wezake huubakilitaja jina langu,
kwa wezake ambao ninaamini hawaijui lugha ya kiswahili tunayo zungumza
"Umetokea wapi?"
"Tanzania dada yangu"
"Ulikuja huku kufanyaje?"
"Wapi, kwani hapa ni wapi?"
Kabla sijajibiwa nilicho kiuliza nikasikia sauti za watu waliomo ndani
ya chumba wakisalimia kwa pamoja kwa kutumia lugha wanayo izungumza,
sauti nzito ya mwanaume ikaitikia na kuwafanya watu wote kukaa kimya
ndani ya chumba tulichopo
"Mumesema, ameamka?"
Mwanaume huyo alizungumza kiswahili cha kuvuta maneo, akionekana kwamba hakifahamu vizuri
"Ndio baba, na anazungumza kiswahili"
"Amesema ametokea wapi?"
"Tanzania, ila hajanitaji ni sehemu gani"
Mwanaume huyo akaendelea kuzungumza kilugha chao, baada ya muda akatoka ndani ya chumba tulichopo
"Eddy baba amrsema tukuache upumzike"
"Ndoja kwanza, unaitwa nani?"
Msichana huyo akakaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akajikoholesha kidogo kuliweka koo lake vizuri kisha akanijibu kwa upole
"Nitakujibu, ukiwa vizuri"
Nikamsikia akitoka ndani ya chumba nilichopo, nikajipapasa kifuani
mwangu, na kukuta kitambaa kigumu kikiwa kimefungwa kuzunguka usawa wa
kifua changu chote
"Ehee Mungu warehema, nisaidie mimi mja wako"
Nilizumgumza kwa sauti ya chini, huku nkihisi machozi yakinitiririka
pembezoni mwa macho yangu.Kumbukumbu za maisha yangu ya nyuma nilipo kua
bado mdogo zikaanza kunijia kichwani mwangu, picha ya sura ya mana
yangu ikaanza kunijia kichwani na iukumbuka baadhinya matukio ya furaha
aliyo kua akinifanyia
'Eddy mwanangu jaribu kuishinda hasira yako'
Nimaneno ya mama, niliyo anza kuyakumbuka vizuei na hili tukio lilitokea
kipindi nilipo mpiga mwenzangu nilipo kua chekechea hadi akapoteza
maisha akiwa anakimbizwa kupelekwa hospitalini
'Usiwe mjinga na wewe utakubali vipi kupigwa na mwanaumwe mwenzio'
Nimanenoya mzee Godwin, alipo kua akinifundisha mbinu za kupigana baada ya kupugwa sana na wezangu nilipo kua darasa la kwanza
'Mwanaume halisi, hupambana hadi dakika ya mwisho ya uhai wake'
'Hata ikiwezekana kutoa roho ya mtu wewe toa tu, ili mradi uwe msindi'
Nimaneno menfine ya mzee Godwin alipokua akinifundisha kadei siku
zilivyokua zikienda jambo ambalo alinifanya na mimi ka katili na roho ya
kinyama tangu nilipo kua mdogo.
'Uwe unasamehe saba mara sabini, kwani Mungu anawasamehe wale wote walio mkosea'
Nimaneno mengine ya mama, alipokua akinifundisha kusoma biblia kabla ya
kulala, kwani alipenda kunikuza katika mazingira ya kidini na kumujua
Mungu
'Mimi baba yako, nihodari sana wa kuua pale ninapo kua kwenye uwanya wa
vita, risasi yangy moja inapo toka kwenye mdomo wa hii bastola yangu,
hua nilazima imuangamize mtu'
Maneno ya Mzee Godwin yakaendelea kujirudia kwenye akili yangu, siku hii
alikua akinifundisha kulenga shabaha kwa kutumia bastola take tukiwa
shambani, tulipo kwenda kuwinda nguruwe pori waliokuwa wakila mihogo
yetu
'Jitahidi kumuomba Mungu mwanangu kwani yeye ndio muweza wa kila jambo, usimruhusu shetani akaitawala roho yako'
Mana alijitahidi kadri ya uwezo wake kunishawushi kuwa kijana mwema.
Maumivu makali yaliyo changanyika na uchungu moyoni mwangu, yakaanza
kunitawala, hapa ndipo nilipo gundua, maisha yangu yameharibika kwa
kufwata maneno ya baba, na kuyaacha maneno ya mama, ambae siku zote
alinihasa niwe kijana mwema, mbaya zaidi baba niliyekua nikimuamini kwa
kila alicho niambia, mwisho wa siku amekuja kya adui yangu namba moja,
hii ni baada ya kugundua kwamba mimi sio mtoto wake, bali ni wapacha
mwenzake
Siku zikasonga mbele nami ndivyo nilivyo zidi kupata unafuu wa machi
yangu, pamoja na kifua changu ambacho kilipigwa baadhi ya risasi na
rafiki yangu John, ikafika kipindi macho yangu yakapona kabisa kutokana
na kutibiwa kwa dawa za kienyeji zilizo nipa uponyaji huu, hapa ndipo
nikaruhusiwa kutoka njie ya nyumba ya nyasi niliyo kuwa nimekaa kwa
kipindi kirefu kidogo, mazingura ya wanakijiji yakanishangaza kwani
mavazi waliyo yavaa, yametengenezwa na ngozi za wanyama, hususani
wanaume, vinguo vyao vya chini, ni ngozi ili juu ya vjfua wapo vifua
wazi.Nikiwa ninaendelea kuwashangaa wanakijiji hawa, ambao nao pia
wanaonekana kunishangaa kwa jinsi nilivyo, jamaa mmoja mwenye misuli
mikubwa na mweusi akanifwata na kwaishara akaniomba nimfwate nyuma,
sikuwa mbishi nikaanza kumfwata huku tukikatiza kwenye mitaa tofauti ya
kijiji hichi chenye nyumba nyingi, zilizo tengenezwa kwa udongo na
kuezekwa kwa nyasi juu ya mapaa yao.Tukafika kwenye moja ya jumba kubwa
lililo zingirwa na wanaume wenye vifuavyenye miraba miine, wengine hasi
miraba sita, mikononi mwao wakiwa wameshika mikuki lamoja na ngao, na
muda wote wakiwa makini na kila iangiae katika jumba hili, lililo jengwa
kwa aina yake
Tukaingia kwenye moja ya ukumbi mkubwa ambao nikakutana na wasichana
wengi walio vifua wazi, hiku sehemu zao za siri zikiwa zimefunikwa kwa
vijingozi vidogo, mikononi mwao wameshika mikia ya simba, na farasi
ambayo wanaitumia kumpepea kila anaye ingia sehemu hiyo.Jamaa
akanionyesha sehemu ya kusimama, akaniacha hapa na kuondoka zake, niliwa
ninaendelea kusimama sauti nzito ya mwanaume nikaisikia ikitokea kwenye
nyumaa ya pazia lililopo kwenye ukumbi huu ikiniita jina langu, akatoka
mwanaume wa makamo, aliye valia ngozi ya chui, mwilini mwake huku
kwenye bega la kushoko kukiwa na kichwa cha chui huyo,
"Unaonekana sasa unaendelea vizuri sio?"
"Ndio kwa sasa ninaendelea vizuri kiongozi"
"Safi ila mimi siitwi kiongozi bali ninaitwa chifu Kambute"
"Chifu KAMBUTE?"
"Ndio, karibu uje kuketi hapa karibu yangu"
Nikapiga hatua hadi kwenye kiti chaje kilicho tengenezwa kwa miti migumu
sana, nikakaa pembezoni mwa kiti cheke kama alicyo niamuru kufanya.
"Kwanza pole kwa yaliyo kukuta bwana Eddy"
"Asante sana chifu Kambute"
"Vijana wangu walikuokota kwenye moja ya mto, ambao naji yake,
yanakwenda kwa mfumo wa maporomoko, ulikutwa ukiwa na hali mbaya
walikuchukua na kukuleta hapa nikawaamuru wakujenge kibanda chako, ili
waganga wangu waweze kukufanyia huduna hadi leo ukapona"
"Asante sana chifu Kambute"
Nilizungumza huku nikipiga magoti chini, kama ishara ya kumshukuru kwa
alicho nifanyia. Akaniruhusu ninyanyuke na kukaa kama nilivyo kaa
mwanzoni
"Nilifurahi sana kusiki kwamba unajua kuzungumza kiswahili fasaha, na pia nilifurahi kusikia umetokea Tanzania"
"Kwa nini Chifu Kambete?"
"Mwaka 1975, baba yangu alinipeleka nchini Tanzania, kwenda
kusoma,ambapo alibikabidhi kwa rafiki yake Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere, kipindi hicho alikua ni raisi wa nchi ya Tanzania"
Ilinibidi nimshangae chifu huyu, kwani ninaimani anaitambua vizuri Tanzania, japo hadi sasa hivi sijijui nipo wapi
"Kipindi hicho cha makaburu hapa nchini Afrika kusini, hakiwaruhusu watu
wengi kupata elimu, na ukibagatika kupata elimu basi ni yamasharti
makubwa inayo fundisha utamaduni wao. Baba yangu alinipeleka kule
kisuri, kutokana alikua ni chifu katika kijiji hichi cha Kambute,
Nilikaa Tanzania kwa Miaka zaidi ya kumi na tano, ambapo, nilibahatika
kuzaa na mwanamke mmoja, alikua akiitwa Maria"
Sauti ya chifu kidogo, ikapungua uzito wake, huku machozi yakianza kunlenga lenga usoni mwake,
"Maeia alikufa, kipindi mwanangu akiwa na umri wa miaka mitatu,
ilinilazimu kurudi naye huku, ambapo nilimkuta baba akiwa katika hali
mbaya sana, naye hakukaa sana alidariki dunia kutokana na magonjwa
yawakumbayo wazee wengi."
Kijistori cha chifu kilinisisimua mwili wangu sikujua ni kwanini ameamua kuzungumza maneno mengi kwangu.
"Pole sana chifu"
"Nimesha poa"
Chifu Kambute, hakuendelea kuzungumza kitu cha aina yoyote zaidi ya
kuondoka na kuagiza nibadilishiwe mavazi nivae kama walivyo vaa wao.
Japo kwangu ni ngumu sana kuvaa nguzo za wanyama kama nguo ili ilinibidi
kufanya hivyo.Taratibu nikaanza kuyazoea mazingira ta watu wa hichi
kijiji, chifu akaniomva niingie kwenye jeshi la kijiji hichi, ambapo
nikaanza kufundishwa taratibu jinsi ya kutumia silaha za asili katika
kupambana, ikiwemo kutumia majambia makali. Nilistushwa na makofi ya mtu
yakitokea nyuma yangu, baada ya kufanya vizuri katika mapambano yangu
na jamaa mmoja miongoni mwa askari katika eneo la kufundishiwa kupigana
"Hongera sana"
Sauti ya msichana huyu haikuwa ngeni sana kwangu, kwani niliisikia
kipindi nilipo kua bado ni mgonjwa wa macho. Msichana huyu ni mrefu
kiasi, huku umbo lake likia limekaa kimazoezi sana, japo ni mrembo
kisura ila mazingira aliyo kiweka ni tofauti sana na mazingira wanayo
jiweka wasichana wanao jijua wai niwarembo, msichana huyu akachomoa
upanga wake, akashuka kwenye farasi aliye mpanda na kuja katika eneo
nililo simama, askari wote wakatuzunguka.
Gafla msichana huyu akaanza kunishambulia kwa haraka kwa kutumia upanga
wake nkali ni mrefu kiasi, ikanilazimu na mimi kujitetea kwa upanga
wangu. Kila nilivyojaribu kujikinga na upanga wangu ila msichana huyu
anaonekana hodari sana katika kutumia upanga, nikastukua akinipiga mtama
na kuanguka chini, huku ncha ya upanga wake ikielekea kwenye koo langu
"Vipi unahitaji kuendelea kupambana?"
Aliniuliza huku akihema sana na jasho lilimwagika kwani mapigano tuliyo
yafanya nimajali kupita maelezo. Kutokana na kuchoka sana sikuwa na haja
ya kuendelea kupambana naye, akanipa mkono na kuninyanyua juu
"Ninaitwa Lutfia"
Alijitambulisha jina lake, nikataka kuzungumza jina langu akanizui
"Unaitwa Eddy, ulisha niambia jina lako"
"Wewe ndio yule uliye, zungumza nami siku ya kwanza?"
"Ndio mimi, ila unahitaji kufanya sana mazoezi, ili kuwa askari mzuri"
Lutfia alizungumza huku akimpanda farasi wake
"Jioni tutaonana nina mazungumzo na wewe"
"Wa....."
Tatari Lutfia alisha ondoka na farasi wake na kuniacha nikiwa
nimeshangaa.Nikarudi katika kibanda changu ninacho ishi, nikakaa kwenye
kitanda changu cha kamba, huku jasho likinimwagika, nikajichunguza msili
wangu nikagundua kuna mabadiliko makubwa sana kwani kifua changu
kimekua kikubwa na kugawanyika kama askari wengine, hii nikutokana na
mazoezi magunu niliyo patiwa kwa kipindi kirefu tangu afya yangu ilivyo
tengemaa
"Kuna haja ya kuondoka, siwezi kuendelea kuishi kwenye mazingira haya"
Nilizungumza mwenyewe, nikaletewa chakula kama kawaida ya mama huyu
anàye niletea chakula.Nikamaliza kula na kuelekea kwenye mto ambao
tunautumia kuoga askari wa kijiji hichi kila ifikapo jioni. Nkawakuta
baadhivya askari wakioga, nikavua kinguo cha kingozi changu, amoja na
upanga wangu ambao muda wote ninatembea nao, nikaingia kwenye mto na
mimi nikaanza kuoga.
Kwa mbali nikamuona Kutfia akiwa amesimama kwenye moja ya kilima
kilichopo karibu na mto huu, nikawatizama askari wote wanao oga
nikawaona wapo bize na stori zao, Lutfia akaniita kwa ishara, nikatoka
ndani ya mto na kuvaa kingozi changu, nikazuga zuga na kuondoka pasipo
askari wezangu kustukia kitu chochote. Nikapandisha hadi eneo alipo
Lutfia, akaniomba nilande kwenye farasi wake, sikusita sana, nikapanda
na kukaa nyuma yake na kuondoka katika ene hili, akanipeleka kwenye moja
ya msitu akamsimamisha farasi wake, sote tukashuka.
"Nifwate?"
Tukaingia ndani zaidi ya msitu, ulio tulia sana ukiwa hauna kelele za viumbe wengine zaidi ya kusikia hatua zetu tunazo tembea.
"Huku ni wapi?"
Lutfia hakunijibu zaidi ya kugeuka na kunitaza, akapiga hatua hadi
sehemu niliyo simama, akanitazama usoni mwangu kwa muda, akaipitisha
mikono yake shingoni mwangu, akauleta mdomo wake karibu na mdomo wangu
ila nikaukwepesha, mdomo wangu, na taratibu nikaichomoa mikono yake,
shingoni mwangu. Nikatoa upanga wangu na kuanza kupiga hatua za
taratibu, kuelekea mbele tulipo kua tunakwenda kwani kuna kitu nilihisi.
Gafla nikastukia kusikia kelele za Lutfia, nikageuka nyuma haraka
nikakuta akiwa ameshikwa na mijitu minne yenye nguvu huku sura zao
zikiwa zimechorwa, kadri nilivyo zidi kuishangaa ndivyo ilivyo zidi
kuongezeka na kufika ya mijtu kumi na saba huku akiwa na marungu makubwa
mikononi mwao
ITAENDELEA
ENDELEA KUDWATILIA SIMULIZI HII, KUPITIA WHATSAPP KWA MALIPO YA SH. 3000 TU KWA MWEZI, NO 0657072588,
NITAKUTUMIA INBOX BAADA YA MALIPO, KAMA ULILIPA PESA YAKO NA HUKUPATA
HUDUMA KWA SABABU ZILIZOPO NJE YA UWEZO WANGU, NITEXT INBOX WHATSAPP,
FACEBOOK NAWE NITAKUHUDUMIA.ASANTE
SORRY MADAM 74
ILIPOISHIA
Gafla nikastukia kusikia kelele za Lutfia, nikageuka nyuma haraka
nikakuta akiwa ameshikwa na mijitu minne yenye nguvu huku sura zao
zikiwa zimechorwa, kadri nilivyo zidi kuishangaa ndivyo ilivyo zidi
kuongezeka na kufika idadi ya mijtu kumi na saba huku akiwa na marungu
makubwa mikononi mwao
SASA ENDELEA
Nikaushika upanga wangu vizuri, nikijiandaa tayari kwa mashambulizi
dhidi ya hii mijitu, iliyo tisha. Tararibu ikaanza kunizunguka, huku
ikiwa imeshika marungu yao kwa umakini.
"Mungu nusaidie"
Nilizungumza kimya kimya huku nikiendelea, kuushikilia upanga wangu
ambao una urefu kiasi. Gafla majitu hayo yakaanza kunishambulia,
kutokana na uzoefu nilio upata dhidi ya kutumia upanga, haikuniwi ugumu
wowote katika kujibu mas uh ambulizi ya kijitu hii, inayo onekana haiña
mbinu kabisà za kupambana, kwani ninajikuta nikiimaliza kijinga kwa
kuikata vichwa vyao
Kwa bahati nzuri, Lutfia akapata nafasi ya kujitoa kwenye mikono ya
mijitu iliyo mkamata, likawa ni zoezi moja tu, lakuhakikisha
tunaishambulia mijitu hii hadi tunaiua yote, kutokana na uhodari wetu
wakupambana, tukafanikiwa kuiua yote, jambo lililo tupa uhakika wa sisi
kuishi
"Eddy umechoka?" Lutfia aliniuliza
"Hapana sijachoka"
"Tuondoke hili eneo si salama"
Tukapanda kwenye farasi, na kuindoka katika eneo tulilo kuwa. Tukàfika
karibu na kijiji, nikashuka kwenye farasi na kumuacha Lutfia atangulie
kududi, ili kuepusha hisia mbaya zitakazo jengwa miongoni mwa
wanakijiji, dhidi yetu.
Nikafika kwenye kijumba changu, sikuingia ndani nikatafuta mti uliopo
karibu na kijumba changu nikapanda, kutokana ni usiku sikuhitaji nilale
ndani, kwani bado nimapema
"Nimepakbuka nyumbani" Nilijisemea kimya kimya
"Nitarudije lakini?”
"Hakuna jinsi nilazima nitoroke hapa ki....."
Nikastushwa na mlio mkali wa king'ora kilichopo hapa kijijini, moti
mkali kutoka kilipo kijiji, ukaniogopesha na kunifanya nikae kwa
umakini, kuchunguza ni nini kinacho endelea, kelele za wamama na watoto
zikazidi kurindina kijiji kizima, huku moto ukiendelea kuteketea. Kwa
haraka nikashuka juu ya mti, nikaanza kukimbia kuelekea kilipo kijiji,
kabla sijafika, nikashuhudia jinsi wanakijiji wanavyo uliwa na watu
wenye bunduki, pamoja na mabomo yakurusha kwa mkono
"Ohhh Mungu wangu!"
Nilihamaki huku nikiwa, sihui chakufanya. Baadhi ya askari wakijiji,
wameanguka chini baada ya kushambuliwa kwa risasi, kitu kiluchozidi
kunichanganya ni baada ya kumuona Lutfia akiwa amezingirwa na watu hao
wenye bunduki nzito na mara nyingi bunduki hizi hutumika kwenye vita vya
mataifa makubwa kama Marekani.
"Upanga hauto saidia chochote"
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiendelea kujibanza kwenye mti mkubwa,
nikishuhudia jinsi wanakijiji wanavyo patishwa matesona watu hao.
Mlio mkali wa helcoptar, ukasikika ukitokea mashariki mwa kijiji,
nikaichungulia Helcoptar hiyo, nikaishuhudia ikitua taratibu sehemu
yenye uwazi, ambapo ndipo walipo kusanywa wanakijiji, pamoja na chifu
wao. Askari mmoja kati ya wengi walio kishambulia kijiji, akakimbilia
hadi sehemu ilipo Helcoptar, akafungua mlango, wa helcoptar.Akashuka
mwanadada mmoja aliye valio nguo nyeusi, kuanzia juu hadi chini, huku
kichwa chake akikivisha kofia nyeusi, huku baadhi ya nywele zake
akizishusha eneo la uso wake na kufucha jicho moja kama anavyo fanya
mwanadada, mwanamuziki Rihana.
Akashuka jamaa mwengine, ambaye naye amevalia nguo nyeusi, kofia pamoja
na miwani nyeusi. Wakapiga hatua hadi, walipo wanakijiji walio wekwa
chini ya ulinzi. Wakaanza kuwakagua wanaume wote, walio amrishwa kupiga
magoti, huku mikono yao wakiwa wamevishika vichwa vyao. Jamaa huyo
akaanza kurusha rusha mikono kama mtu aliye changanyikiwa, baada ya
kukagua wanaume wote, akaivua kofia yake na kuitupa chini.
Nikastuska, baada ya kuiona sura ya mtu huyu, ambaye usoni mwañgu si
mgeni sana japo jiña lake, bado halinijii kichwani kisawasawa, akamfwata
chifu, aliye pigishwa magoti kwa amri ya wa ajeshi hao. Akaichomoa
bastola yake kiunoni na kuielekezea kichwani mwa chifu
Kutokana na umbali waliopo sikuweza kusikia nimaswali gani anayo muuliza
çhifu, anaye kuwa mbishi kujibu, gafla nikamuona Lutfia akimsukuma
jamaa huyo aliyekuwa akihitaji kumfyatulia baba yake risasi, kwa jinsi
vitendo anavyo vifanya Lutfia, vinaashiria kumuimba jamaa huyo,
amuadhibu yeye na si baba yake.
Jamaa akamtandika Lutfia kichwani, kwa kutumia kitako cha bastola yake,
nakumfanya chifu anyanyuke kwa hasira, kabla hajamkabili jamaa huyo,
msichana aliye shuka naye kwenye Helcoptar, akafyatua risasi kadhaa
zilizo muangusha chifu chini kama gogo kubwa.
"God...!"
Niligamaki, huku nikimshuhudia Chifu, anavyo tapatapa chini, akikata
roho, askari mmoja wa kijiji akajaribu kunyanyuka, ila akarudishwa chini
kwa risasi, alizo pigwa kwenye miguu yake. Jamaa akachukua kipaza sauti
na kuanza kuzungumza
"Natambua upo hapa kijijini, nipo hapa kwa ajili yako, rafiki yangu kipenzi Eddy"
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio hukunikijiiza swali, ni kwanini hawa watu wapo kijijini kwa ajili yangu.
"Hutaki uje tupige stori? Njoo basi rafiki yangu Eddy. John nipo hapa ninakusubiri"
Hasira ikazidi kuyaongeza kasi mapigo yangu ya moyo, picha kadha
kichwani mwangu zikaanza kujirudia kwa kasi, kama mkanda wa video, unao
rudishwa nyuma. Picha za kumbukumvu zikasimama, katika tukio la John,
kunipiga risasi za kifua baada ya mke wangu Phidaya kujifungua, miguuni
mwangu
"Ohhhh Eddy, hutaki? Basi ngoja niondoke zangu.Ila kabla sija ondoka nina ujumbe kutoka kwa mke wako na mwanao Jimy"
Maneno ya John yakazidi kunichanganya, sikua na lakufanya kwabi askari
wake wapo zaidi ya hamsini na wote wana bunduki mikononi mwao.
"Mke wako, na mwanao wanakuhitaji rafiki yangu. Ndio maana nikaamua kuja
kukutafuta, baada ya kusikia upo hài. Kaka mimi na wewe ni marafiki wa
damu. Tafadhalu njoo twende nyumbani, ukamuone Jimy wako"
Maneno ya John yaliyo jaa ushawishi, wakibinadamu sikuyapa nafasi katika
kichwa changu, kwani asinge fanya alicho kifanya kwa wanakijiji wezangu
"Ohhh ngoja nimpigie simu, umsikie mkeo"
John akatoa simu yake mfukoni, akaiweka sikioni mwake kwa sekunde kadhaa, kisha ajaisogeza karibu na kipaza sauti chake
"Mume wangu Eddy, ninakupenda sana.Nimeishi mbali nawe kwa miaka mitatu
sasa, ninakuomba urudi nyumbani, mwanao ananisumbua kila siku kusema
baba, baba."
"Nakuomba Eddy wangu, urudi. Ngoja nimsikilizishe mwanao simu. Jimy talk to dady"(....Jimy zungumza na baba)
"Halloo Dady, where are you? I mis you. Came back home"(Halloo baba, upo wapi? Nimekukumbuka, rudi nyumbani)
Sauti ya mtoto mdogo ilisikia vizuri masikioni mwangu, jambo lililozidi
kunitatiza nakunipa wakati mgumu sana, japo sauti ni yamke wangu Phidaya
ila sikufanya maamuzi yoyote kwenye kichwa changu
"Muambiw baba, umekua wa kwanza darasani"
Sauti ya Phidaya ilimuamrisha mtoto huyo anaye semekana niwakwangu
"Dady nimekua first in class"
Mtoto, alichanganya kiswahili na kingereza, jambo lililo nipa wasisi wa
kuhisi kuna kamchezo kanacho endelea katikati yao. John akakata simu na
kujikoholesha kidogo
"Eddy umesikia hiyo. Mke wako, mwanao, wote wanakuhitaji wewe. Njoo twende zetu rafiki yangu"
John alizungumza huku akitazama kila pande ya eneo walilopo, akitarajia
kuniona, tarativu nikajikuta nikikaa chini, huku machozi yakinimwagika.
Nikautazama upanga wangu kwa umakini, kisha nikachungulia walipo,
nikamuona John akikikamata kitoto kimoja chenye umri wa miaka kama
mitatu
"Eddy mwanao anafanania na huyu"
John ilizungumza huku akimbembeleza bembeleza mtoto huyo, anaye lia kwa
sauti ya juu, hii ni baada ya kutolewa kwenye mikono ya mama yake aliye
lazwa chini
"Eddy muda unakwenda, njoo tuondoke. Sasa hivi ni saa saba usiku.
Unasubiri ninj rafiki yangu. Au unataka ukae na hawa watu wako, walio
vaa nusu uchi eheees?"
John aliendelea kuzungumza huku, akizunguka zunguka katika eneo
walilopo, mkononi akiwa na mtoto aliye endelea kupaza sauti ya mayowe.
Gafla John akamgeuza mtoto, kichwa chini, miguu juu, huku akiwa amemshika kwa mkono mmoja, mguu wakulia.
Kitendo cha John kumshika, mtoto huyo hivyo, kikanikumbusha jinsi Derick alivyo mshika mtoto wangu, niliye zaa na Madam Mery.
"Eddy hujui ni jinsi gani, ninavyo chukia kupotezewa muda. Huku mijitoto
inayo lia kama hii, inavyo zidi kunicchanganya akili yangu"
John akakitupa kipaza sauti chini, pasipo kua na huruma, akachomoa
bastola yake na kuzimimina risasi kadhaa tumboni mwa mtoto huyo, na
kumtupa chini kama mzoga
"Fuc......"
Nilizidi kupandwa na hasira iliyo ufanya mwili wangu wote kutetemeka.
Vilio vya wamama vikazidi kuutesa moyo wangu, nikamuona John akikiokota
kipaza sauti, huku akicheka kwa dharau
"Ohhhhh Eddy, naondoka, ila hili ulilo liona linakwenda kumkuta mwanao Jimy"
John akamrushia kipaza sauti, msichana aliye kuja naye, naye akamkabidhi
askari mwengine kipaza sauti. Wakaondoka, wakaingia kwenye Helcoptar
yao na kuondoka.
Askari wao wakaondoka kwa umakini, na kutokomea pasipo julikana.
Nikasubiri kwa muda, wa nusu saa, ndipo taratibu nilipo anza kutembea
walipo wanakijiji wanao omboleza kwa machungu, vifo vya wapendwa wao.
Kila mwanakijiji anaye niona, ananitazama kwa macho makali yaliyo jaa
jazba.
Macho yangu yakakutana na macho ya Lutfia, aliye pembeni ya mwili wa
baba yake, aliye fariki dunia. Nikatembea kwa haraka hadi ulipo mwili wa
chifu, kabla sijaugusa, nikastukia, Lutfia akinisukuma kwa nguvu na,
nikaanguka chini
"Eddy, hupaswi kuugusa mwili wa baba yangu. Haya yote wewe ndio chanzo. Umekisababishia kijiji changu matatizo...."
"Lutfia ila si mimi niliye waua hawa wote"
"Wewe, ni chanzo Eddy, nakuanzi sasa hivi ninakuomba uondoke kijijini
kwangu, la sivyo utakwenda kuungana na kifo cha hawa wote walio tangulia
mbele za haki"
Lutfia alizungumza kwa msisitizo, huku machozi yakimwagika, ñà kifua
chake kikipanda na kushuka kwa kasi akionekana kujawa na jazba kubwa
dhidi yangu.
ITAENDELEA
WASILIANA NAMI KUPITIA 0657072588/0768516188. PIA NICHEKI INSTAGRAM @eddy_msulwa NAKUTAKIA SIKU NJEMA
ILIPOISHIA
Macho yangu yakakutana na macho ya Lutfia, aliye pembeni ya mwili wa
baba yake, aliye fariki dunia. Nikatembea kwa haraka hadi ulipo mwili wa
chifu, kabla sijaugusa, nikastukia, Lutfia akinisukuma kwa nguvu na,
nikaanguka chini
"Eddy, hupaswi kuugusa mwili wa baba yangu. Haya yote wewe ndio chanzo. Umekisababishia kijiji changu matatizo...."
"Lutfia ila si mimi niliye waua hawa wote"
"Wewe, ni chanzo Eddy, nakuanzi sasa hivi ninakuomba uondoke kijijini
kwangu, la sivyo utakwenda kuungana na kifo cha hawa wote walio tangulia
mbele za haki"
Lutfia alizungumza kwa msisitizo, huku machozi yakimwagika, ñà kifua
chake kikipanda na kushuka kwa kasi akionekana kujawa na jazba kubwa
dhidi yangu.
ENDELEA SASA
"Lu....."
"Eddy nimesema ondoka"
Lutfia alizungumza kwa kupaza sauti, hadi wanakijiji wote wakatutizama
sisi, natambua hawajui lugha tunayo izungumza ila, matendo yanaashiria
kwamba Lutfia hataki kuniona mbele ya macho yake. Nikamtazama Chifu,
huku machozi yakinilenga lenga. Midomo ya Lutfia, inatetemeka kwa kufura
kwa hasira, uzuri wake alio kua nao umetoweka kabisa. Taratibu
nikauweka chini upanga wangu, kisha nikasimama na kutazamana na Lutfia
aliye nitumbulia mimacho kiasi cha kunifanya nimuogope. Kila mwana
kijiji ninaye mtazama sura yake imetawaliwa na majonzi mengi, wamama
wengine wakiwa wanalia kwa uchungu huku wakigara gara kwenye vumbi,
wakionyesha ni jinsi gàni, walivyo umizwa na tukio zima lililo tokea
muda mchache ulio pita.
Sikumuangali mtu yoyote usoni zaidi ya kugeuka na kuanza kutembea kwa
mwendo wa haraka, ulio changanyika na hasira kali. Nikafika kwenye
kijumba changu, nikachukua kibuyu changu, ninacho hifadhia maji ya
kunywa, nikachukua na kisu changu cha akiba, na kutoka nje ya kibanda
changu. Nikautizama mji jinsi unavyo teketea kwa moto, hasira dhidi ya
John ikazi kunipanda. Nikaanzà kutokomea msituni, nikijaribu kutafuta
njia ya kutokea kwenye kijiji hiki, kutokana na hasira pamoja na uchungu
ulio nitawala moyoni mwangu, nikajikuta nikitembea hadi kuna pambazuka,
pasipo kuchoka.
Nikafika kwenye moja ya mlima mrefu, ulio zingirwa na miti mingi, kwa
mbali nikaanza kusikia mngurumo wa gari, likipita eneo la karibu na
mlima huu, kwa haraka nikashuka, nikiufwatisha mgurumo huo ni wapi unapo
tokea. Kwabahati nzuri nikaiona barabara ya lami, iliyo chongwa kwenye
mlima huu. Matunaini ya kufika ninapo pahitaji yakaanza kunijia moyoni
mwangu.
Nikasimama, katikati ya barabara. Sikuona aibu kwa jinsi nilivyo vaa
nusu uchi, huku sehemu zangu za siri, zikiwa nimezifunika na ngozi ya
chui. Mlio wa gari sikuusikia tena, kwani ninahisi lilisha pita, kabla
ya mimi kuifikia barabara. Nikaendemea kuzunguka zunguka maeneo ya
barabara, nikijaribu kusubiria kama ninaweza kupata usafiri.
Gafla gari moja ndogo, likapita kwa kasi pasipo kufanikiwa kulipungia
mkono, ila halikufika mbali sana, likasimama. Dereva wa gari hilo
akaanza kulirudisha nyuma kwa kasi, hadi sehemu nilipo simama. Kioo cha
upande wa dereva kikashuka, nikamuona mvulana mmija wa kizungu, àkiwa na
mchumba wake, wakabaki wakinishangaa kwa jinsi nilivyo vaa.
Binti wa kizungu akatoa kamera yake, aina ya digital, na kuanza kunipiga
picha, huku akiwa amesimama upande wa lili wa gari, nikaanza kuwafwata
taratibu
"Casey get in the car"(Casey ingia ndani ya gari)
Mvulana huyu, alizungumza kwa haraka baada ya mimi kilikaribia gari lao,
kabla hajafanya chochote, nikawahi kuingiza mkono kupitia upenyo wa
kioo alicho kifungua. Nikachomoa funguo ya gari lao, nakulifanya lizime.
Jamaa akashuka, huku akiwa amekasirika, akajaribu kunirukia, ila
nikamuwahi kumtuliza kwa ngumi ya shingo iliyo muangusha chini na
kuzimia hapo hapo.
Msichana akajaribu, kukimbia ila nikamuwahi na kumdaka, nikambeba begani
na kumrudisha ndani ya gari. Nikachomoa kisu changu na kumuwekea kooni
mwake huku kidole changu kimoja kikimpa ishara ya kukaa kimya la sivyo
nitamkata kichwa. Nikaufunga mlango wake, ña kuzunguka upande wa pili,
sehemu alipo anguka mpenzi wake. Kwa haraka nikamvua nguo mpenzi wake,
na kuzivaa mimi japo hazinitoshi sana ila nikazilazimisha kukaa mwilini
mwangu.
Nikachukua soksi za jamaa, na kumkandamiza nazo mdomoni, kisha
nikamnyanua na kufungua, uoande wa pili wa gari. Kwa bahati nzuri
nikakuta kamba, kwa haraka nikamfunga miguuni na mikononi. Kisha
nikamuwena vizuri nyuma ya gari, hii yenye viandishi vidogo vilivyo
andikwa Verosa, kisha nikafunga, nikarudi alipo mpenzi wake.
Nikamkuta akihangaika na simu yake, akijaribu kupiga namba anazo zijua
yeye, kwa bahati mbaya, maeneo tuliyopo hakuna mawasiliano.
Nikampokonya simu yake na kuiweka mfukoni mwangu
"Ukijaribu kufanya ujinga wowote, nitakuu"
Nilizungumza kwa sauti ya ukali nikitumia lugha ya kingereza, jambo
lililo mfanya binti huyo kushangaa, kwani nahisi alijua kwamba mimi ni
mtu misiye jua lugha yoyote zaidi ya lugha ya jamii niliyo tokea
Nikawasha gari na kuondoka, huku mara kwa mara niki muamrisha binti huyu
kunielekeza barabara ya kufika kwenye mji wowote. Mwendo wa karibia
masaa tisa, tukafika kwenye moja ya mji wenye nyumba, nyingi sana zilizo
tengenezwa kwa mbao
"Hapa ni wapi?"
"Soweto"
Casey alinijibu kwa kifupi huku, akiwa amenuna, kwani hajafurahishwa na
uwepo wangu mimi, ndani ya gari hili. Nikasimamisha gari nje ya baa
moja, iliyo tulia sana,
"Mbona umesimamisha gari?"
"Nahisi njaa, nahitaji kula, nipatie pesa"
Casey akanitazama kwa woga, taratibu akaingiza mkono wake kwenye, mfuko
wa suruali aliyo ivaa, akatoa noti moja ya dola mia na kunikabidhi,
nikafungua mlango, kabla sijashuka, nikamgeukia Casey.
"Shuka ndani ya gari, tuongozane"
Casey hakuwa na kipingamizi zaidi yakushuka kwenye gari, tukaingia ndani
ya baa hii kwa bahati nzuri tukakuta, sehemu wanauza chakula
"Wewe unaitwa nani?"
Casey aliniuliza kwa sauti ya chini, huku tukiendelea kukisubiria chakula tulicho kiagiza
"Eddy"
"Una jina kama la mchumba wangu"
"Yupi, huyo niliye mfungia kwenye buti ya gari?"
"Hapana, huyo ni kaka yangu, mpenzi wangu yupo hospitali"
"Anaumwa na nini?"
"Alishambuliwa na majambazi, wiki moja iliyo pita"
"Ohoo pole saña, ila hali yake inaendeleaje?"
"Sio nzuri, kwani yupo chini ya uangalizi wa madaktari, kwani alipigwa risasi nne za kifua, alipokua anapeleka pesa benki"
Casey alizungumza kwa sauti yaunyonge huku kwambali nachozi yakimlenga
lenga, tukachukua chakula tulicho kiagiza na vinywaji, tukarudi kwenye
gari
"Eddy nakuomba kitu kimoja"
"Kitu gani?"
"Ninakuomba umfuñgulie kaka yangu, nahisi atakuwa anajihisi njaa"
Casey aliniomba kwa utaratibu, nikamtazama kwa umakini, machoni mwake
Nikamkabidhi mfuko wa chakula nilicho kishika, nikazunguka nyuma ya
gari, nikajifikiria kwa muda kisha nikakishika vizuri kitasa cha
kufungulia buti ya gari.
Kabla sijafungua, gari ya polisi, ikasimama nyuma yangu, jambo lililo nifanya nisitishe zoezi, nikaanza kuondoka, nyuma ya gari
"Hei kijana"
Sauti ya askari mmoja ikaniita, nikageuka kwa kujiamini, na kuwatazama
askari wawili walio simama mbele ya gari lao, dogo linalo endana na gari
ninalo liendesha.
"Njoo"
Nikapiga hatua kurudi walipo, askari hawa walio zichomeka bastola zao viunoni mwao
"Fungua, buti ya gari. Tunahitaji kukagua gari yako"
Alizungumza askari mmoja huku akinifwata sehemu bilipo simama, nikaanza
kuchanganyikiwa baada ya Casey kushuka ndani ya gari na kuja tulipo
"Ofisaa"
Casey alimuita askari mmoja, aliye simama akitutiza, Casey akanitazama
kwa macho makali, jambo lililo wafanya askari hao kuipeleka mikono yao
kwenye bastola zao walizo zichomeka viunoni.
ITAENDELEA
WASILIANA NAMI KUPITIA 0657072588/0768516188. PIA NICHEKI INSTAGRAM @eddy_msulwa NAKUTAKIA SIKU NJEMA
SORRY MADAM 76
ILIPOISHIA
"Ofisaa"
Casey alimuita askari mmoja, aliye simama akitutiza, Casey akanitazama
kwa macho makali, jambo lililo wafanya askari hao kuipeleka mikono yao
kwenye bastola zao walizo zichomeka viunoni.
ENDELEA
Nikataka kurudi nyuma, ila nikajikuta miguu ikipata uzito wakutekeleza
azma yangu ya kurudi nyuma. Askari wakazichomoa bastola zao, kwa haraka
wakatusukuma mimi na Casey, tukaanguka chini.
"Laleni chini"
Askari mmoja alizungumza kwa sauti ya juu huku akianza kutambaa,
wakielekea ilipo baa, tuliyo toka muda mchache. Milio ya risasi ikaanza
kurindima, ndani ya baa, nikatazama vizuri, nikashuhudia kundi la
majambazi walio valia makofia meusi vichwani mwao, yaliyo bakisha sehemu
za macho yao, wakiwamrishà watu waliomo ndani ya baa hiyo kutoa walivyo
navyo.
Ikawa kama mkanda wa kuigiza, kwani majambazi hao walianza kuwashambulia
askari hao walio kua wakitambaa, mmoja wao, akapigwa risasi ya kichwa
na mmoja wa majambazi, na ukawa ndio mwisho wa askari huyo, aliyetoka
kuzungumza na Casey muda mchache ulio pita.
Nikamtazama Casey, na kumuona akijaribu kunyanyua kichwa chake
kuchungulia upande walipo majambazi hao, na akaanza kupiga mayowe yaliyo
wafanya majambazi kutazama eneo lilipo gari, letu.
"Weka kichwa chako chini, Casey"
Nilizungumza kwa sauti ya ukali, huku nikibingiria kwa haraka, na
kumuwahi Casey aliyekuwa ameshikwa na butwaa, akimshuhudia askari aliye
zungumza naye, jinsi ubongo wake ulio changanyikana na damu, ulivyo
sambaa chini.
"Heiii, nisikilize wewe"
Nilizungumza huku nikimpiga piga Casey mashamvuni, ili arudi katika hali yake ya kawaida.
"Eheeee!"
Alizungumza huku akiwa amenitumbulia mimacho, asijue nini azungumze.
Gari yetu ikaanza kushambuliwa kwa risasi na majambazi hao, huku sisi
tukiwa upande wa pili wa gari hili. Nikatazama upande lilipo gari la
polisi, nikachungulia kupitia durisha la gari, tulilopo nikao majambazi
wawili wakilisogelea gari letu huku wakiendea kuzimimina risasi kwenye
upande wa pili wa gari letu.
"Hei Casey, unaweza kutambaa?"
"Heee"
"Unaweza kutambaa?"
Casey akanijibu kwa kutingisha kichwa kwamba anaweza.
"Nakuomba, utambae uende lilipo gari lapolisi"
"Eddy una akili kweli wewe, unataka na mimi nife kama hao polisi?"
Casey alizungumza kwa sauti ya kuto kujiamini huku akinitazama usoni, huku jasho likimtiririka.
"Fanya kama nilivyo zungumza"
Nilizungumza, huku nikiwachunguli majambazi hao, wanao zidi kulisogelea gari letu lilipo.
Casey hakuwa na uchaguzi mwengine zaidi yakufanya nilivyo muambia
kufanya. Kwa haraka akatambaa hadi lilipo gari la polisi na kujibanza
huku akihema sana, macho yake yote yakawa kwangu. Ukimya ukatawala
gafla, kwani majambazi waliacha kupiga risasi, nikachungulia nikawakuta
wakinong'onezana, mmoja akaanza kunyata taratibu, akilisogelea gari
nililopo, huku bunduki yake akiwa ameiishika vizuri mkononi mwake.
Nikakichomoa kisu changu, na kukishika kwa mkono wangu wa kulia.
Taratibu nikanza kuhesabu moja mpaka tatu, kitendo cha jambazi huyo
kuufungua mlango wa gari, upande wa dereva, ikawa ninafasi yangu kufanya
shambulizi la kukirusha kisu changu kwa nguvu zangu zote, kisu changu
kikatua shingoni mwa jambazi aliye simama, hatua chache toka gàri
lilipo, akatoa ukelele ulio mduwaza mwezake, aliye karibu yangu. Kwa
haraka nikapanda juu ya gari, nikajizungusha kwa kasi, kwakuitumia miguu
yangu, na kumpiga kichwani jambazi, akaanguka chini. Nikawahi kuochomoa
bastola iliyo kiunoni mwake, na kumpiga risasi kadhaa za tumbo.
Nikakimbia kwa haraka, hadi kwenye moja ya gari, lililopo kwenye
maegesho ya hapa baa, nikajibanza kutazama ni kitu gani kinacho endelea
ndani ya baa. Jambazi mmoja akajitokeza mlangoni kuwachungulia wezake,
alipo waona wamelala chini, akarudi ndani kwa haraka, sekunde kadhaa
wakatoka majambazi wanne, wakaanza kufyatua risasi zao ovyo, pasipo
kujua muhusika mkuu wa mauaji ya wezao wawili yupo wapi.
Sikuhitaji kufanya makosa, ambayo yangenigharimu maisha yangu. Kwa
haraka nikanza kufyatua risasi zilizo wapeleka chini, majambazi wote
wanne, Nikatoa magazini ya bastola, nikskuta imebakiwa na risasi nne tu.
"Shitii"
Nilizungumza huku nikiirudisha kwa harana Magazine hiyo ndani ya
bastola, nikanyanyuka kwa umakini, nikaanza kukimbilia katika mlango wa
kuingilia baa.
Nikachungulia na kuwakuta watu wote wakiwa wapo chini ya ulinzi mlali wa
majambazi sita waliomo ndani ya baa hii, iliyo kusanya wateja wengi.
Jambazi mmoja, akajisumu kutoka nje, nikamrukia kwa nyuma na kumkaba
kabali, huku nikimvuta pembeni kabisa ya mlango. Taratibu jambazi huyu
akaanza kuiaga dunia, kwa nguvu zangu zote nikaivunja shingo yake.
"Nisalimie huko uendapo"
Nikamlaza chini, taratibu nikachukua bunduki yake àina ya 'Short Gun',
Nikamvua jaketi lakuzuia risasi alilo livaa, nikaanza kushangaa baada ya
kuguñdua jambazi huyu ni mwanamke.
Nikalivua kofia lililopo kichwani mwake, sikuamini macho yangu, kwani ni binti mdogo sasa, jinsi anavyo onekàña usoni mwake.
"Umekosa nini, binti mzuri kama wewe?"
Nilizungumza huku nikilivaa jaketi la kuzuia risasi. Kazi ikawa ni moja
tu, kuhakikisha ninawamaliza mambazi wote. Haikuwa ngumu kwangu, kwani
ndani ya dakika kadhaa nikafanikiwa kuwaua majambazi wote ndani ya baa
hii. Mtu mmoja akaanza kupiga makofi, mwenzake wa pembeni naye akafanya
hivyo, watu wote waliomo ndani ya baa wakaaendelea kunipigia makofi kwa
kazi nzuri niliyo ifanya.
"Asanteni"
Nilizungumza, kwa kizulu jambo lililo zidi kuwafurahisha, walio na simu
zao wakawa na kazi ya kunipiga picha, huku wengine wakichukua video.
Casey akanifwata na kunikumbatia, huku akitokwa na machozi
"Vipi?"
Nilimuuluza kwa wasiwasi, huku kitu cha kwanza kukifikiria kichwani
mwake ni kaka take, niliye muacha ndani ya buti ya gari lililo
shambuliwa vibaya kwa risasi.
"Umeyaokoa maisha yangu"
Casey alizungumza huku akiendelea kulia
"Casey tuondoke"
Sauti ya kaka yake ilisikika, na kutufanya sote tutizame mlangoni na
kumkuta àkiwa amesima, huku akiwa na nguo ya ndani tu. Akajistukia
mwenyewe baada ya watu wote, kumshangaa.
"Naweza kupiga simu?"
Casey alimuuliza mmoja wa wahudumu aliye valia sare kama wahudumu wengine
"Ndio"
Casey akaonyeshwa simu iliyo kwenye moja ya ukuta ndani ya hii baa,
akaniachia na kwenda kupiga simu, baada ya kumaliza akarudi nilipo
simama
"Nimempigia simu baba, atafika muda si mrefu"
Ving'ora vya gari za polisi vikafika katika eneo la tukio
"Kumbe hawa nao hawana tofauti na wabongo"
Nilijisemea kimoyo moyo, huku nikiwatazama askari hawa wakiingia kwa
mbwembwe ndabi ya baa hii huku, wakiwa na bunduki mikoni mwao
"Weka silaha yako chini"
Askari mmoja aliniamrisha huku, wakinielekezea bunduki zao.
Nikashangaa wazee wawili wakisimama mbele yangu huku, mikononi mwao wakiwa wameshika chupa za bia.
"Nyinyi muda wote mulikua wapi? Huyu kijana yeye ndio aliye waua majambazi wotw hawa, bila aibu munakuja sasa hivi"
"Kwanza hamshangai, jinsu tulivyo mzingira huyu kijana, munadhani ni jambazi?"
Wazee hawa walipokezana kuwatandika maswali askari hawa, walio baki
wakibabaika wasijue nini chakuwajibu wananchi hawa waliopo ndani ya hii
baa. Askari wakaachana na mimi, wakaanza kushuhulika na miili ya
majambazi hao. Kundi kubwa la waandishi wa habari walio kuja baada ya
askari kufika, wakaanza kunihoji naswali ambayo sikuyajibu hata moja.
"Eddy baba yangu amekuja"
Casey alizungumza huku, akinishika mkono na kutoka ndani ya baa.
Nijakuta gari nne , nyeusi zinazo fanana, aina ya GVC, zika zimejipanga
pembeni, huku zikiwa na vijibendera vidogo vya marekani. Walimzi wapatao
kumi, walio valia suti nyeusi, pamoja na miwani nyeusi, wakashuka
kwenye magari hayo. Kaka yake Casey akaongoza zilipo gari hizo, huku
mkononi mwake akiwa ameshika kamera ya Casey, akashuka mzee mmoja mwenye
mvi kichwani mwake.
"Eddy yule ni baba yangu"
Casey alizungumza huku akiendelea kunishika mkono nielekee zilipo gari hizo.
"Ngoja kwanza, siwezi kwenda kwa baba yako nikiwa kwenye halii hii"
"Wewe twende baba yangu hana tatizo"
Casey alizungumza huku akiendelea kunivuta, tukafika zilipo gari zao, akakumbatiana na baba take.
"Baba, huyu ni shujaa aliye yaokoa maisha yangu. Anaitwa Eddy"
"Eddy huyu ni baba yangu, ni balozi wa Marekani, hapa Afrika kusini"
Nikampa mkono, baba Casey naye akaupokea wa kwangu huku akiachia tabasamu pana.
"Asantw kijana kwa kazi nzuri uliyo ifanya"
"Asante mzee"
Casey akamuomba baba yake niweze kujumuika nao kwenda wanapo ishi,
ikawalazimu walunzi kunikagua, mwili wangu kamakuna kitu kinaweza
kuwadhuru. Wakachukua bastola yangu, wakaniruhusu kuingia ndani ya gari.
Sikupanda gari moja na Casey na baba yàke, gari nililo panda likari
wawili walio kaa siti ya mbele mmoja akiwa ni dereva. Kwangu ikawa kama
bahati kukutana na balozi huyu wa Marekani. Japo mama yangu ni waziri wa
nchini Tanzania, ila sikuweza kubahatika kukutana ni viongozi wa nchi
kubwa kama Marekani. Katika siti niliyo kaa, nyuma ya siti ya dereva
kuna Tv ndogo inayo onyesha, vipindi mbalimbali. Matangazo ya kituo cha
television kinacgo itwa ENEWS, kikaanza kuonyesha tukio la majambazi
walio kufa, huku ikisadikika kundi hilo la majambazi lilikuwa
likitafutwa na jeshi la polisi la Afrika kusini, zaidi ya miaka mitano
sasa, pasipo mafanikio.
'NI MTU MMOJA TU, AMEWEZA KULISAMBARATISHA KUNDI HILO HARAMU'
Nimaneno ya mtangazaji wa taarifa hiyo, huku picha za video zikinionyesha, walivyo kua wakinihoji.
"Wewe ni askari?"
Mlinzi mmoja aliniuliza, pasipo kugeuka nyuma kunitazama
"Hapana"
"Umewezaje kutumia silaha?"
"Nilifundishwa na baba yangu, yeye alikua ni mwanajeshi"
"Yupo wapi?"
"Amesha kufa"
Nilidanganya, huku nikiangalia saa ndogo iliyopo pembezoni mwa dereva,
ikionyesha ni saa sita usiku. Nikageza shingo yangu kutazama pembezoni
mwa barabara, ambapo kuna bonde kubwa na endapo dereva akikosea basi
tukianguka, huko bondeni tutakua tutasagika sagika bibaya,na isitoshe
gari zote zipo kwenye mwendo kasi sawa kwa uzoefu wangu, spidi wanayo
tembelea ni zaidi ya spidi mita mia moja. Matone matone ya mvua yakaanza
kutotesha vioo vya gari letu tulilo panda, ambalo ni lapili kutokà
mbele, kati ya msafata wa magari manne yaliyo ongozana. Kitu ninacho
wasifu madereva hawa, ni utaalamu wao kukunja kona, bila kupunguza
mwendo wa magari yao, zilizopo kwenye hii bararaba iliyo chogwa
kitaalamu, pembezoni mwa mlima ninao weza kuufanan uliopo mkoani Iriñga
ni Tanzania.
Nikiendelea kuitadhimini barabara hii, gafla nikastukia kuliona gari la
mbele yetu, nikinyanyuliwa hewani na kitu kama bomu kutegwa, likazunguka
hewani mara kadhaa na kutua chini, kitendo kilicho mfanya dereva wetu
kufunga breki za gafla, zilizo lifanya gari kuserereka na kuligonga gari
lililo anguka na kulisukumia bondeni, kwenye korongo refu, huku matairi
ya mbele ya gari letu yakianza kutangulia kwenye korongo, huku ya nyuma
yakijitahidi kubaki barabarani.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 77, SHARE NA LIKE HII POST. 0657072588 KWA MAELEZO ZAIDI.
SORRY MADAM 77
ILIPOISHIA
Nikiendelea kuitadhimini barabara hii, gafla nikastukia kuliona gari la
mbele yetu, nikinyanyuliwa hewani na kitu kama bomu kutegwa, likazunguka
hewani mara kadhaa na kutua chini, kitendo kilicho mfanya dereva wetu
kufunga breki za gafla, zilizo lifanya gari kuserereka na kuligonga gari
lililo anguka na kulisukumia bondeni, kwenye korongo refu, huku matairi
ya mbele ya gari letu yakianza kutangulia kwenye korongo, huku ya nyuma
yakijitahidi kubaki barabarani.
ENDELEA SASA
Macho yangu yote, yakahamia kwenye gari inayo kuka nyuma yetu kwa kasi
kubwa, huku dereva wake akijitahidi kufunga breki zake, akitumia juhudi
zake zote
Nikajiluta nikiyafunga macho yangu, kwani kitu kinacho fwata sekunde
chache, ni dereva huyo, kutusindikiza kwenye korongo kama alivyo fanya
dereva wetu, kwenye gari lilil kua mbele yetu.
Dakika kama mbili, hivi niliendelea kusikilizia ni nini kitatokea,
kwetubila haikuwa hivyo. Mwanga mkali wa taa za gari lililo kua nyuma
yetu, ukaendelea kunipiga machoni, ni sentimita chache sana, toka lilipo
simama gari lililopo nyuma yetu, huku gari letu, likianza kunesa
taratibu.
"Tutulie hivi hivi"
Dereva alizungumza huku akihema sana, askari walio kwenye magari ya
nyuma wakashuka kwa haraka, kwenye magari yao, wakaja nyuma ya gari letu
na kuanza kujitahidi kulivuta kwa nyuma. Kutokana na uzito wa gari
ikawa ni kazi ngumu sana kwao kulivuta. Ikawalazimu kulishikilia na
kutuomba tushuke haraka.
Sikutaka nipoteze muda, nikaufungua mlango wa nyuma katika siti niliyo
kaa na kutoka nje haraka iwezekanavyo, huku walinzi nilio kua nao ndani
ya gari wakitokea kupitia mlango nilio pitia mimi.
Walinzi wakaliachia gari, likaporomoka kwenye korongo. Nikiwa ninatazama
huku na kule, nikawaona watu wakiwa juu kidogo ya mlima wakijipanga kwa
ajili ya kufanya shambulizi
"Shitiii"
Bila hata ya kuomba, nikachomoa bastola moja ya mlizi aliyo ichomeka
kiunoni mwake. Nikafyatua risasi mbili kwa jamaa aliye shika bunduki
aina ya 'Snaiper' ambayo ni hatari sana, kutokana na uwezo wake mkubwa.
Mashambulizi yakaanza rasmi, na watu hawa ambao ndio walio tegesha
bomu barabarani. Ikawa ni ambushi moja ambayo hakuna aliye itarajia kama
inaweza kutokea kwa wakati huu, askari wawili wakapigwa risasi na kufa
hapo hapo.
"Gari la balozi ni lipi?"
Nilimuuliza mlinzi mmoja, niliye simama naye karibu, tukiendelea kujibu
mashambulizi ya wavamizi hawa, ambao wanapig a risasi kama wendawazimu
"Lile la mwisho"
"Nilinde"
Jamaa akaendelea kuwafyatulia majambazi risasi, huku mimi nikikimbia
pembezoni mwa kuta ya mlima huu, jambo lililo gumu kwa majambazi kuweza
kuniona. Nikafika lilipo gari la balozi, nikamkuta akiwa ameinama kwenye
siti yeye pamoja na wanae, wakimuomba Mungu wao
"Muheshimiwa unaniamini?"
Nilimuuliza balozi mara baada ya kuingia ndani ya gari na kukaa, katika siti ya dereva.
"Ndio nakuamini."
Kutokana gari halikuzimwa, likanirahisishia wepesi wa kufanya jaribio la
kumuokoa balozi pamoja na familia yake. Nikaangalia upenyo ulio achwa
na gari, lililo simaba barabarani, nikaamini unanitosha kupita.
Mlinzi akanipa ishara nipite, yeye anaendelea kupambana na wavamizi
hawa. Nikafanya kama alivyo agiza, kalilazimisha gari kupita kwenye
uwazi wa gari lililopo barabani, chakushukuru Mungu likapita, ikawa kazi
ni kwangu kuhakikisha ninasonga mbele.
Japo kuna risasi kadhaa zilipigwa kwenye gari letu, ila hapakuwa na
iliyo adhiri matairi zaidi ya kuvunja vioo vya pembeni. Kwa mwendo kasi
wa gari hili, ulinifanya niwe makini kwa kila kona ninayo kunja
barabarani.
"Ohhh Mungu wangu! tunafwatwa nyuma"
Kaka yake Casey alizumgumza huku, akichungulia kwenye kioo cha nyuma
kilicho jaa matundu ya risasi. Sikutaka hata kutazama nyuma kuzihofia
kona za papo kwa papo, huku nyengine zikiwa ni kali sana.
"Wapo wangapi?"
”Pikipiki mbili na gari ndogo tatu"
"Muheshimiwa unaweza kutumia, silaha?"
"Eheee?"
Balozi alibabaika kwenye kunijibu swali nililo muuliza. Sikuwa na jinsi
zaidi ya kuongeza mwendo kasi wa gari, ninalo liendesha. Tukafanikiwa
kuingia kwenye barabara iliyo nyooka, hapa ndipo nikapata wakati mzuri
wa kuwatazama wanao tufwata kupitia kioo changu cha pembeni.
"Hawa vijana ni kina nani?"
"Siwajui muheshimiwa"
Waendesha pikipiki, nikawaona wakilikaribia gari letu, kutokana na mwendo wao mkali. Nikapunguza mwendo taratibu
"Mbona unapunguza mwendo?"
Balozi aliniuliza huku akitetemeka, hata sauti yake haikutoka vizuri
"Najua nini, nafanya"
Nilimjibu kwa kujiamini, huku macho yangu yote yakiwa kwenye kioo cha
pembeni nikiwatazama jinsi majambazi hao wakija kwa kasi, Nikakanyaga
breki kwa nguvu zangu zote, huku nikilizungusha gari kwa mtindo wa
duara, jambo lililo wafanya waendesha pikipiki hawa kulivaa gari letu,
na kila mmoja akarushwa vibaya na kuangukia upande wake wa barabara.
Kutokana na uhodari wa gari hili, halikuweza kuyumba wala kuzima. Ila
kilicho, niogopesha ni jinsi gari ilivyo geuka na kutazama tulipo tokea
ambapo kuna gari mbili ndogo zinatufwata, na mbaya zaidi zipo karibu
kutufikia.
Ikanilazimu kulirudisha gari kinyuma nyuma ili nipate, japo nafàsi la kuligeuza, nitakavyo jua mimi.
Nikiwa ninaendelea kurudi nyuma kwa mwendo wa kasi japo si sana
nikaliona, gari tulili liacha sehemu tuliyo vamiwa likaja kwa kasi nyuma
ya gari hizi mbili ndogo, zinazo tukimbiza.
"Ohhh wamelichukua hata hili"
Nilizungumza huku nikijitahidi kupata nafasi ya kuligeuza gari hili, ila
kwa bahati mbaya upande nilio kuawepo mimi kuna gari kubwa la mizigo,
likija kaa kasi huku dereva wake akijitahidi kunipigia honi, nimpishe
upande wake, lasivyo anatugonga.
Nikalirudisha kwa haraka upande wa kushoto ambapo ndipo ninapo stahili
kupita, dereva wa gari ambaye alikuwa upande mmoja na mimi, nikastukia
akigongana uso kwa uso na gari hilo la mizigo, tukio lililo mstusha
mwenzake ambaye nipo naye upande mmoja. Akajikuta akifunga breki, bila
hata ya kutegemea gari lililo kuwa nyuma yake, likamvaa na yote kwa
pamoja yakatoka nje ya baranara huku yakizunguka, na kutimua vumbi
jingi, huku vyuma vya magari yao vikisagika ikiashiria kwamba yana
gongonga kwenye mawe makubwa yaliyopo pembezoni mwa barabara.
Nikakanyaga breki, kusimamisha gari. Nikashusha pumzi nyingi, huku nikilitazama vumbi likielea angani.
"Kila mmoja yupo salama?"
"Ndio"
"Ndio"
"Ndio"
Kila mmoja alijibu kwa wakati wake, nikatazama upande wa mbele tulipo
tokea, sikuona gari lolote likija, saa iliyopo pembeni yangu inaonyesha
ni saa kumi na moja alfajiri. Taratibu nikaliemdesha gari hadi, hadi
zilipo gari hizi mbili.
"Bakini ndani ya gari"
Nilizungumza kwa kujiamini, nikaichukua bastola yangu niliyo kuwa
nimeiweka pembeni mwa siti, niliyo kalia. Nikafungua mlango wa gari na
kushuka, huku nikiwa makini sana na tayari kwaa lolote litakalo jitokeza
mbele yangu.
Nikafika ilipo gari ndogo, na kumkuta dereva akiwa amelalia mskani wake,
ulio mbana maeneo ya kifuani. Nikamchunguza na kugundua bado anahema
kwa shida, huku damu zikimtoka puani na mdomoni.
"Ni...ss..aid..ie"
Aliniomba msaada huku akinitaza kwa macho yaliyo mtoka. Mithili ya mtu aliye kwabwa na kitu kizito kooni.
"Nani aliye kutuma?"
"Nisa....i..die...ni.tamtaj...
.a"
Nikaikoki bastola yangu kuziandaa risasi kutoka, kidole changu kimoja
kikianza kuivuta traiga, taratibu, huku nikiwa nimemuelekezea bastola
kichwani kwake.
"Nakuuliza kwa mara ya mwisho. Ninani aliye watuma?"
Jamaa alipo litazama shimo dogo, la kutolea risaai la bastola, akayarudisha macho yake usoni mwangu.
"J....oh..n"
Jamaa, alinijibu kwa shida kubwa sana, na kichwa chake kikalegea,
akiashiria ameiaga dunia. Kwa hasira nikamsindikiza huko aendapo kwa
risasi moja iliyo tua kichwani mwake.
Nikasikia sauti ya mtu akikohoa kwenye gari, tulilo liacha sehemu ya tukio.
Nikaanza kutembea kwa umakini, huku bastola yangu nikiishikilia
vizuri, nikamkuta yule amlinzi tuliye muacha eneo la tukio, akiwa amekaa
chini huku ameliegemea gari, mkono wake mmja akiwa amejishika tumboni
mwake, kunapo vuja damu nyingi, sura yake ikiwa imechanika chanika kwa
kuchwana na vipande vya vioo vya gari.
Alipo niona akatabasamu kidogo, huku akikohoa na kumwaga madonge ya damu mdomoni mwake.
"Muheshimiwa yu..po salama?"
"Ndio yupo salama"
Nilimjibu, huku nami nilipiga goti chini, nikijaribu kumtazama ni nini kilicho mpata sehemu ya tumbo.
"Asante kwa msaada wako, wewe ni mwanaume shujaa."
Alizungumza huku, akitabasamu na kukohoa juu.
"Damu nyingi, imenitoka. Suwezi pona"
Alizumgumza maneno haya baada ya kujaribu, kumpa huduma ya kwanza. Akanishika mkono wangu wa kulia
"Toa pochi yangu, kwenye......mfuko wa nyuma"
Nikaitoa pochi, akaniomba niifungue na kitu cha kwanza kukiona na kitambulisho chake chenye jina la George Jr.
"Fungua, upande wa pili"
Nikafungua na kukuta, picha mbili moja akiwa mdogo na nyingine akiwa
amesimama na msichana aliye nifanya niitumbulie mimacho picha hiyo.
"Chukua hii chane, naomba umtafute dada yangu anaitwa Victoria, umkabidhi hii cheni."
George Jr. Alinikabishi cheni aliyokua ameivaa shingoni mwake. Huku
taratibu, akianza kuyapepesa macho yake. Akanyayua mkono wake taratibu,
huku alitetemeka, akanipigia saluti na kukata roho.
Taratibu machozi yakaanza kunimwagika, nikayafunika macho yake kwa
kupitia kiganja cha mkono wangu wa kulia. Nikageuka nyuma, nikamkuta
baloIi akiwa amesimama na watoto wake, huku Casey machozi yakimwagika.
Nikanyanyuka taratibu, na kwenda lilipo gari na kuingia. Nikaitazama
picha ya George aliyopiga na Victoria. Nikajikuta donge la hasira
likinibana kifuani mwangu.
Nikasikia milio ya helcoptar, nikawasha gari kaa haraka, ila Casey akanikimbilia
"Eddy tupo, salama hao ni wanajeshi wa Marekani, wanakuja"
Casey alizumgumza huku, akichungulia dirishani. Helcoptar mbili
zikashuka hewani na kusimama, katikati ya barabara. Wakashuka wanajeshi
wengi, wenye bunduki mikononi. Balozi akaanza kuzumgumza nao, huku kaka
yame Casey, akipewa nguo ajisitiri mwili wake.
Wakatuchukua, sote wanme na kuondoka huku, Helcoptar nyingine ikibaki, na wanajeshi kadhaa wakiupima pima mwili wa George Jr.
Tukafika makao, makuu ya jeshi la Marekani lililopo hapa, nchini Afrika
kusini. Tukapewa huduma za kwaza ikkwemo vifungua kinywa, kwani hatukupa
chakula kwakipindi kirefu. Matumbo yalipo kaa sawa, nikatambulishwa mm
wa baadhi ya wakuu wa jeshi. Wengi wao wakanisifu kwa kazi nzuri na
pevu, niliyo ifanya.
Tukapelekwa kwenye moja ya hoteli kubwa, tukiwa chini ya uangalizi
mkali wa jeshi. Balozi Brayan Daniel, hakusita kunitambulisha kwa kila
rafiki yake ambaye, huku akinimwagia sifa kedekede. Tukakaa hotelini,
kwa siku nne, ambapo Balozi Brayan Daniel akaendelea na majukumu yake ya
kazi, huku akiniomba niwaliende watoto wake kwa kipkndi kifupi kabla
hatujaenda Marekani, kuhudhuria mazishi ya askari walio kumbwa na tukio
la uvamizi.
Mida ya saa sita mchana, ikafika gari katika hoteli tuliyopo, huku
akija muwakilishi wa balozi, akituomba twende ofisini kwake, tukakutane
na baadhi ya viongozi wa hapa nchini Afrika kusini. Tukajiandaa, kila
mmoja akavalia mavazi tuliyo numuliwa siku kadhaa, tumaingia ndani ya
gari, huku mimi nikiwa makini kuhakilisha Casey na kaka yake wapo salama
salmini.
Tukafika kwenye ofisi za ubalozi wa Marekani, tukapokelewa vizuri na
kupelekwa kwenye ofisi za balozi, ambapo tulimkuta yupo na watu baadhi,
wanao onyesha kua ni viongozi. Tukakaa kwenye viti vilivyo andaliwa kwa
ajili yetu.
"Jamani mutatiwia radhi kidogo kwa kuchelewa kufika kwenye halfa hii"
Sauti ya John, ilisikika kutokea mlangoni, akiingia akiwa ameongozana na
Victoria, mpenzi wake.Pasipo kutazama waliopo ndani ya ofisi John na
Victoria, wakakaa kwenye viti vyao na kukamilisha idadi ya watu ishirini
na tano, tuliomo humu ndani, Nikaivua miwani yangu nyeusi niliyo ivaa,
nikamuona John, akilegeza mdomo wake kwa kunishangaa, huku naye Victoria
akiinamisha kichwa chini kwa aibu, wasiju nini cha kufanya. Huku
nikiwakazia macho yaliyo jaa hasira kali kama Simba.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 78, YA SIMULIZI HII YA KUSISIMUA. WASILIANA NAMI SIMU NO 0657072588. USIKAE MBALI NA PAGE HII KWANI KUNA OFA KABAMBE, ITAKUJIA HIVI KARIBUMI NA SI YAKUKOSA.
SORRY MADAM 78
ILIPOISHIA
Pasipo kutazama waliopo ndani ya ofisi John na Victoria, wakakaa kwenye
viti vyao na kukamilisha idadi ya watu ishirini na tano, tuliomo humu
ndani, Nikaivua miwani yangu nyeusi niliyo ivaa, nikamuona John,
akilegeza mdomo wake kwa kunishangaa, huku naye Victoria akiinamisha
kichwa chini kwa aibu, wasiju nini cha kufanya. Huku nikiwakazia macho
yaliyo jaa hasira kali kama Simba.
ENDELEA SASA
Ukimya wa sekunde kadhaa, ukakatiza huku macho yangu nikiyahamisha
kutoka kwa John, kwenda kwa Victoria. Swali la kwanza kujiuliza ni
kuhusiana na John anahusika kivipo kwenye huu mkutano, hiyo moja mbili
anamahusiano gani na balozi wa Marekani bwana Brayan Daniel.
"Nashukuru kwa kufika kwenu, kwa maana nyinyi ni wachache kati ya wengi nilio tamani wafike hapa."
Balozi B.Daniel alizungumza huku akiwa amesimama.
"Lengo langu la kuwaita hapa, ndugu zangu, ni kumtambulisha shujaa wangu, aliye jitolea kuyaokoa maisha yangu na familia yangu.”
"Huyu ninaye mzungumzia hapa si mwengine bali ni Eddy Godwin."
Balozi alininyoonyea mkono, watu wote wakapigaiwemo Jonh na Victoria.
"Japo nimepatwa na pigo, lakuwapoteza vijana wangu, kumi katika
shambulio lile, Ila kusema ukweli ni jbo la kumsukuru sana Mungu, kwa
kijana Eddy kujitokeza na kuweza kuitetea nafsi yangu. Pasipo kujali
yeye ni nani, ila ni kitu kikubwa sana kufanywa na mtu wa kawaida."
Kila muda ulivyo zidi kwenda, ndivyo nilivyo jikuta nikizidi kupandwa na
hasira kali, hata yañayo zungumzwa ndanivya hichi chumba sikuweza
kuyasikia hata kdogo.
Matukio baadhi aliyo yafanya John, yakanza kunisumbua akilini mwangu,
taratibu nikajikuta nikitokwa na machozi ya uchungu sana. Casey
akaniangalia kwa muda, kwa haraka akanifwata nilipo kaa
"Eddy una tatizo gani?"
Watu wote wakabaki wakitutizama mimi na Casey. Mapigo ya moyo hayakusita
kunienda mbio hadi nikaanza kujihisi kizungu zungu. Nikaanza
kujishangaa, baada ya kuona jinsi matone ya damu yakianza kunitoka puani
"Muiteni dokta"
Nikajaribu kunyanyuka, ila kizunguzungu kikali, kikaniyumbisha kabla sijaenda chini, Casey aksniwahi, akisaidiana na kaka yake.
Macho yakaanza kujaa ukungu mwingi ulio nifanya niwaine watu wawili
wawili. Nikamuona John, akitabasamu. Huku akinyanyuka kwenye kiti alicho
kikalia.
"Tupeni nafasi, tumuhudumie."
Sauti za madkari, nilizisikia kama sauti ya kengele zinazo gongwa.
"Nakufa"
Nilizungumza kwa sauti ya chini, sana, huku nikizidi kujihisi vibaya.
***
Nikastuka gafla, kabla sijanyanyuka, nikastukia nikirudishwa chini, kitandani na dada mmoja aliye valia mavazi meupe.
"Tulia kaka yangu."
"Nipo wapi?"
"Hospitali"
"Kwañi ninaumwa?"
"Ndio"
Nikatizama pembeni, nikaona dripu la maji likishusha kiwango cha maji
kwenye, mishipa ya mkono wangu wa kushoto, kupitia mrija wake mwembamba
ulio unganishwa na sindano yake na kuchomwa kwenye sehemu ya kukunjia
mkono.
"Unajisikiaje?"
"Vizuri"
"Basi tulia, dripu hili likiisha, unaweza kuruhusiwa"
"Litachukua muda gani?"
"Mmmmm masaa kama mawili hivi, kwani ndio nimekuwekea muda huu"
Nikajichnguza mwili wangu, na kujikuta nikiwa na mavazi niliyo yavaa,
mchana. Saa ya ukutani inaonyesha ni saa moja jioni. Nesi akatoka ndani
ya chumba, dakika jadhaa akaingia Casey na kaka yake.
"Unaendeleaje Eddy?" Çasey alizungunza.
"Nipo poa"
"Pole kaka Eddy"
"Asante Bruño"
"Baba yupo, na daktari, wanazungumza kuhusiana na tatizo lako"
"Daktari amesema nina tatizo gani?"
"Amesema kwamba, una...."
Bruno akamziba Casey mdomo asizungumze, anacho taka kukisema kwa muda huu.
"Hapana kaka Eddy, huna tatizo mwaya."
Nikatabasamu huku nikimtazama, Bruno na Casey, nikatambua kwamba kuna tatizo tu, ila nahisi wameambiwa wasizungumze.
"Mbona umemziba mwenzako mdomo?"
"Hapana, anapenda kuongea ongea sana huyu."
"Si uniaçhe, nizungumze.."
Bruno akamziba tena mdomo, Casey na kujikuta wakianza kugombaba, kama jawaida yao.
"Heii jamani acheni kugombana”
Casey akatoka chumbani kwa hasira na kuubamiza mlango. Bruno akaachia
msunyo mkali na kukaa katika sofa lililomo ndani ya hichi chumba.
"Bruno hivi, mbona unapenda kugombana na Casey?"
"Ahaa domo lake, lipo wazi sana"
"Sawa, hivi yule jamaa aliye ingia, baada ya sisi kufika una mfahamu?"
"Yule ndio nina mfahamu, ni rafiki mkubwa sana wa baba"
"Tangu lini?"
"Kivipi yani?"
"Namaanisha wamejuana lini?"
"Tangu mwaka jana, tunakuja hapa Afrika kusini, tukitokea Marekani."
"Ahaaa"
"Tena yule John, ana roho nzuri sana. Haswa yule mke wake."
"Chanzo cha baba, kua rafiki na yule John. Walitoa Hotel yao sisi kuishi
tangu tunakuja hadi tulipo pewa nyumba, tuliyo andaliwa. Kwani balozi
aliye pita kabla ya baba, alifariki kwa ajali ya ndege."
"Kwa hiyo vitu vyake havikuamishwa, kwenye ñyumba tunayo ishi, sasa
hivi. Ikatulazimu kuishi Hotelini, John akajitolea hoteli yake tuishi
bure kwa kipindi chote"
"Ahaaa"
"Hata ile Hotel tunayo kaa sasa hivi ni ya John na mke wake"
"Kweli?"
"Ndio"
"Kumbe nimatajiri dana ehee?"
"Ndio nimatajiri sana, ila nasikia kwamba utajiri wao ni wakuridhi, kutoka kwa baba yake Victoria, ambaye kwa sasa ni marehemu"
Nikastuka, huku nikimtazama Bruno, akili yangu ikaenda moja kwa moja
katika tukio walilo lifanya John na Victoria kutaka kumuua baba yangu.
"Huyo baba yake, Victoria anaitwa nani?"
"Kwakeli simfahamu, ila nilisikia kwamba baba yake alijinyonga, chumbani kwake. Inasadikika alikuwa na ugonjwa wa kichaa"
Nikahisi mwili wangu, ukisisimka, kwani John amechukua, kila kitu kwenye
maisha yangu. Kuanzia mali za baba yangu. Hadi familia yañgu.
Muda wa kuruhusiwa, ukawadia. Daktari akaniomba azungumze na mimi.
Tukaingia ofisini kwake na kukaa kwenye viti vilivyomo humu ndani.
"Tumekufanyia uchunguzi wa kina, tukakukuta na matatizo mawili kwenye
mwili wako. Endapo hayata fanyiwa uharaja wa matibabu, unaweza kupelekea
kifo chako. Bwana Eddy."
Daktari alizungumza huku akinitazama machoni mwangu. Wasiwasi haukuacha kunitawala usoni nwangu.
"Ninaumwa na nini Daktari?"
"Tatizo la kwanza, ni hasira iliyo pitiliza kiwango. Ambayo ikikupanda
sana, inapelekea mfumo wako wa mapigo ya moyo kukuenda kasi sana. Moyo
unapeleka kasi damu kwenye mishipa mbali mbali mwilini mwako. Na ndipo
kuna baadhi ya damu, zinatoka puani mwako."
"Ukishindwa kujizuia hasira yako, itapelekea mishipa ya damu kupasuka, hapo utakua ni mwisho wako wa kuishi duniani"
"Tatizo la pili, tumegundua kwamba, unayemelewa na ungonjwa wa Saratani, ya damu."
Nikahisi mwili mzima ukifa ganzi, kwani sikifikiria kama nitaumwa nà ugonjwa wa Canser, tena ya damu
"Ila usiwe na wasi, nimezungumza na muheshimiwa, utakwenda kufanyiwa
matibabu Marekani. Na saratani itakwenda kupona, kwani ndio ipo kwenye
hatua za mwanzoni mwanzoni."
Daktari akanikabidhi dawa, za kunywa pale nitakapo jihisi vibaya.
"Siwezi kufa hadi nirudishe, kila kitu alicho kichukua John kutoka mikononi mwangu.”
Nilizungumza kimoyo moyo huku, nikitoka chumba cha daktari, nikajumuika na balozi, pamoja na wanae kurudi hotelini.
***
Siku mbili, zikapita na hali yangu ikazidi kuimarika. Kila asubuhi
nikawa na jukumu la kufanya mazoezi, ili kuuimarisha mwili wangu. Nikiwa
nimevalia nguo za mazoezi, raba pamoja na earphone, nikibrudika kwa
mziki, kupitia Ipad aliyo nipa Casey, jana usiku. Nikaendelea kukimbia
barabanani, huku saa yangu ya mkononi, ikinionyesha ni saa kumi na moja
alfajiri.
Katika barabara ninayo kumbia, hakuna wa watu wengi, zaidi ya mtu mmoja
mmoja, ninao kutana nao wakifanya mazoezi kama mimi ya kukimbia.
Nikamkuta dada mmoja aliye vali, suti ya kijivu, Akionekana
kuchanganyikiwa, kwani gari lake analo liendesha, limepata pacha tairi
la mbele.
"Samahani kaka"
Aliniita baada ya kumpita kidogo, nikavua earphone zangu, na kugeuka kumsikiliza ahahitaji kuzungumza na mimi kitu gani.
"Ndio"
"Nakuomba, unisaidie kubadilisha tairi la hili gari."
Nikamtazama juu hadi chini, pasipo kumjibu chochote. Nilipo ridhika na udadisi wangu, nikamsogelea.
"Kwani ilikuaje?"
"Nimekuta tu tairi, likiisha upepo"
"Toa hilo jengine"
Akazunguka nyuma ya gari lake kwa haraka, akatoa tairi pamoja navifaa
vingine vya kusaidia kubadilishia tairi la gari. Nikaanza kazi ya
kulifungua tairi lenye pancha, huku yeye akiwa na kazi ya kunibadilisha
kila spana nitakayo muomba anipatie.
Haikuchukua muda sana, nikamaliza kumfungia tairi lake jipya.
"Asante sana"
"Usijali"
Akafungua mlango wa upande wa dereva, na kutafuta kitu. Kutokana
sikuhitaji kulipwa, nikaanza kuondoka babla sijapiga hatua hata sita
nikasikia akiniita.
"Kaka subiri uchukue zawadi yako"
Nikageuka, sikuamini macho yangu kwani, nikakutana na bastola aliyo ishika huyu dada, akinielekezea mimi
"Tulia hivyo hivyo, ukijaribu kupiga hatua nitakufumua ubongo wako."
Alizungumza huku akiwa ameishika, bastola yake kwa mkono mmoja, huku mkono mwingine akiwa na simu.
"Ninaye hapa"
Alizungumza kupitia, simu yake. Wala sikujua ànazungumza na nani. Mbaya
zaidi siwezi fanya chochote kutokana hii barabara imenyooka sana, na
haina sehemu ya kujificha. Gari nne nyeusi, zenye muundo wa gari kama
zinazo bebea pesa za mabenki, zikafunga breki katika eneo tulilopo.
Wakashuka watu walio valia ñguo nyeusi, makofia meusi yaliyo waficha
sura zao, na kubakishs macho yao tu. Kila mmoja mkononi mwake ameshika
bundiki, na wote wakanizungu huku wakinitazama kwa umakini.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 79. WASILIANA NAMI KWA SIMU NO 0657072588 AU 0768516188.
SORRY MADAM 79
ILIPOISHIA
Gari nne nyeusi, zenye muundo wa gari kama zinazo bebea pesa za mabenki,
zikafunga breki katika eneo tulilopo. Wakashuka watu walio valia ñguo
nyeusi, makofia meusi yaliyo waficha sura zao, na kubakishs macho yao
tu. Kila mmoja mkononi mwake ameshika bundiki, na wote wakanizungu huku
wakinitazama kwa umakini.
ENDELEA
Mmmoja wao akatoa amri ya mimi kuiamsha mikono yangu juu, nikatii
pasipo kubishana. Akatoa amri nyingine ya mimi kulala chini, hapo ndipo
nilipo anza kuleta ubishi, kwani siwezi kukamatika kirahisi.
Kitendo cha mimi kusogeza mguu nyuma, nikastukia kitu chenye ncha kali
kikinichoma mgongoni, kwa haraka nikaupeleka mkono wangu nyuma, kwa
ajili ya kukichomoa. Nikakuta ni sindano
yenye dawa, iliyo anza kuvinyong'onyeza viungo vyangu vya mwili.
Taratibunikajikuta nikianza kuishiwa na nguvu. Nikaanguka chini, kila
nilipo jaribu kunyanyua hata mkono sikuweza, nikajikuta nikiwatazama
watu hao walio nikaribia na kuninyanyua. Nikastukia kitu kizito
kikinipiga, kichwani, giza kali likanitawala machoni mwangu.
********
"Eddy.... Eddy"
Nisauti nyororo, iliyo anza kuisikia taratibu, ikipenya masikioni
mwangu. Taratibu nikayafungua macho yangi, nikakutana na sura ya kike,
huku kichwa chache kikiwa kimejaa nywele nyingi nyeusi na zilizo ndefu
sana.
Macho yake makubwa kiasi, na yadura kiasi, yaliendelea kunitazama huku akiwa ameniimamia, kutoka katika kitanda nilicho kilala.
"Karibu tena duniani" Alizungumza huku akiwa ametabasamu.
"Duniani?"
"Ndio duniani"
"Kwani nilikua, sipo duniani?"
Hakuzungumza chochote zaidi ya kusimama, pembeni ya kitanda nilicho lala.
"Kwa jina ninaitwa dokta, Agines, nimtaalamu katika maswala ya saikolojia"
"Ngoja, hapa ni wapi?"
"Upo Washinton DC, Marekani"
"Ahaaaa?"
"Usishangae, ninaimani kwamna unatambua, nitukio gani ulilo lifanya kwa
ajili ya hii nchi, nasi tumeamua kukuweka karibu nasi na kukusaidia kwa
kila jambo"
Akafungua pazia, kubwa lililopo kwenye moja ya ukuta, hapa ndipo nilipo
anza kuona majengo makubwa yaliyopo katika mji huu, ambapo ndipo yalipo
makao makuu ya serikali ya nchi ya Marekani.
"Tutahakikisha tunakufanyia kila unacho kihitaji"
Akaniandalia chakula, akaniomba nile.
"Ukimaliza kula, kuna watu nitahitaji uonane nao"
"Wakina nani?"
"Utawaona tuu"
Nikamaliza kula, akanionyesha bafuni, nikaoga na kurudi kitandani, huku nikiwa nimejifunga taulo.
"Unaweza kuvaa"
"Mbele yako?"
"Kwani kuna tatizo lolote, tambua kwamba mimi nitakuwa pamoja nawe kwakipindi cha siku tisini"
"Za nini?"
"Eddy vaa bwana, watu hao wanakusubiri."
Nikamtazama kwa muda, nikavua taulo, nikachukua nguo moja baada ya nyingine alizo zipanga kwenye kitanda.
"Umependeza sana"
"Asante"
"Upo tayari"
"Ndio"
Tukatoka ndani ya chumba, hichi kilicho tengenezwa kwa mfumo wa
wakisasa, tukaingia ndani ya lifti na kushuka chini, hapa ndipo nilipo
gundua ghorofa tuliyokuwa ni ya hamsini kutoka chini.
Tukafika chini, kabisa tukaongozana hadi nje ya ghorofa hili, tukakuta
gari karibia sita zenye muundo mmoja wa milango sita zikitusubiri sisi.
Tukaingia kwenye moja ya gari, na gari zote zikaondoka.
"Tunapo kwenda ni wapi?"
"Ahaaa utapaona usiwe na wasiwasi"
Akanipa glasi iliyo jaa whyne
"Ninaamini unatunia hiki kinywaji?"
"Ndio"
Nikaendelea kutazama jinsi mji huu ulivyo jengeka, kwa majengo marefu.
Tukafika kwenye mojo ya geti kubwa, gari zote zikaingia kwa pamoja.
Tukashuka mimi na Agie, tukapokelewa na mdada mmoja aliye valia suti
nyeusi. Akatupeleka kwenye moja ya meli, iliyo simama pembezoni mwa
bahari
"Ni nani huyo tunakwenda kuonana naye?"
"Eddy mbona una haraka, utamuona tu"
Tukaingia ndani kabisa ya meli hii ya kifahari, kila niliye mtazama
alionekana kutabasamu. Wengine wakadiriki kunisalimia, kwafuraha.
"Tuingue humu chumbani"
Tukaingia kwenye moja ya chumba kilicho humu ndani ya meli hii. Tukakuta baadi ya watu wanao onekana ni wanamitindo.
Wakanichukua vipimo vya mwili wangu, wakaanza kunishonea nguo ya mtindo nilio uchangua kati ya mitindo mingi, waliyo nionyesha.
"Agie mbona, mimi sielewi?"
"Huelewi nini Eddy?"
"Mambo yote haya, munanifanyia kwa maana ipi?"
"Eddy kama nilivyo kuambia, inatupasa kulufanyia kitu kama kukulipa fadhila ya uliyo fanya kwa raia wa Marekani"
"Hata kama, ila bado haijaniingia akilini!"
"Kwa nini?"
"Ni watu wangapi, walikufa kwa ajili ya wamarekani muliwafanyia hivi?"
"Ndio ila kila mmoja ana bahati na nafasi yake kwenye maisha. Kwahiyo nafasi yako no hii"
Ndani ya lisaa, nguo niliyo hitaji kushonewa ikawa imekamilika, wakanipa
niijaribu, kutokana na uzoefu wao, hawakukosea kitu hata kimoja.
"Ni muda wakutoka kwenda kukutana na watu nilio, kuahidi utaonana nao"
Nikashusha pumzi huku nikimtazama Agie, ambaye naye, alibadilisha nguo alizo kuja nazo na kuvalia gauni, refu jekundu.
Tukatoka tukiwa tumeshikana mikono, sauti yakiume, kupitia kipaza
sauti nikaisikia ililitaja jina langu, ukumbi wote ukafura kelele za
makofi. Watu walizidi kushangilia huku wakianza kuimba wimbo wa Happy
birtday, wakiashiria ni siku yàngu ya kuzaliwa.
Agie akanipeleka hadi mbele ya ukumvi kwenye sehemu iliyo nyanyuka
kidogo. Kwa matatizo yalivyo nizonga, hata siku yangu ya kuzaliwa
sikuikumbuka.
Ukimya ukatawala ndani ya ukumbi, huku watu wakinisubiri nizungumze kitu chochote.
"Kipindi, nilipo kuzaa, nilitambua kwamba ipo siku utakuja kua mtu muhimu kati ya watu wengi ulimwenguni humu"
Sauti ya mama, ilinistua, kupitia vipaza sauti vilivyomo humu ndani, nikatazama pande zote za ukumvi ila sikumuona mama.
"Usipate shida ya kunitafuta, nipo hapa mwanangu"
Nikamuona mama, akisimama katikati ya watu huku mkononi mwake akiwa ameshika kipaza sauti.
"Leo maombi yàngu, Mungu ameyasikia. Nilikutafuta kwa miaka mingi mwanangu. Hadi leo nimekuona"
Mama alizungumza huku akipiga hatua akija mbele nilipo, mashafu ya mama
yakaanza kujaa machozi, yanayo mtiririka kutoka machoni mwake.
"Umekua mwanangu, hadi leo unatimiza miaka ishirini na tato, kweli umekua mwanangu"
Nikashikwa na kigugumizi hata sikuweza kuzungumza, mama akanikaribia na
kunitazama usoni mwangu, nami nikashindwa kuyazuia machozi yangu.
Tukajikuta tukikumbatiana kwa pamoja na kuwafanya watu, waliopo ukumbini
kupiga makofi
"Nakupenda sana mwanangu, Eddy"
Sikutarajia kama ninaweza kukutana na mama yangu, baye nimepotezana naye kwa kipindi kirefu sana
"NA...KU..PENDA PIA MAMA"
Nilizungumza huku, machozi yakinimwagika, yakiendana na sauti iliyo jaa
kigugumizi. Kati ya watu walio simama ukumbibi, nikamuona Sheila,
akipiga makofi huku akimwagikwa na machozi ya furaha
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 80, HAPA HAPA KWENYE UKURASA WA STORY ZA EDDY.
SORRY MADAM 80
ILIPOISHIA
Tukajikuta tukikumbatiana kwa pamoja na kuwafanya watu, waliopo ukumbini kupiga makofi
"Nakupenda sana mwanangu, Eddy"
Sikutarajia kama ninaweza kukutana na mama yangu, baye nimepotezana naye kwa kipindi kirefu sana
"NA...KU..PENDA PIA MAMA"
Nilizungumza huku, machozi yakinimwagika, yakiendana na sauti iliyo jaa
kigugumizi. Kati ya watu walio simama ukumbibi, nikamuona Sheila,
akipiga makofi huku akimwagikwa na machozi ya furaha
ENDELEA SASA
Taratibu mama akaniachia na kunibusu kwenye paji la uso wangu.
Akasimama pembeni yangu nakuniomba nizungumze chochote, kwa watu walio
nifanya sasa hivi kuwa na furaha.
"Siamini, kitu ninacho kiona mbele ya macho yangu."
Nilizungumza huku nikijifuta machozi yafuraha yanayo nimwagika usoni mwangu.
"Sina kitu kingine chakuzungumza zaidi ya kusema asanteni, nyinyi nyote. Mulio nikutanisha na familia yangu. Asanteni sana."
Nikamapa kipaza sauti, muendeshaji wa shughuli hii, mama akaninishika
mkono na kunipeleka kwenye moja ya meza, iliyo na kitu kikubwa kilicho
funikwa na kitambaa cheupe.
"Eddy tunakuomba ufunue hicho kitambaa"
Muongozaji wa shughuli alizungumza nami nikafanya kama alivyo zungumza.
Sikuamini kuona keki kubwa, iliyo tengenezwa kwa muonekano wangu.
Nguo zilizo tengenezwa kwenye, keki hii, ni zile nilizo kua nimezivaa
siku nilivyo kua katika mapambano, ya kumuokoa balozi wa marekani na
familia yake, huku mkononi nikiwa nimeshika bastola. Wadada wawili walio
valia sare nzuri za suti zenye rangi ya 'cream' wakasimama karibu yangu
na kuanza kuikata kekii hii, yenye maandishi yaliyo andikwa kwenye
kibao cheusi ambacho nacho pia ni keki, yanayo someka
(Wewe nishujaa wa maisha yangu na familia yangu, hongera kwa siku yako ya kuzaliwa)
Wakamaliza kukata vioande vya keki, kisha muongoza sherehe akaniomba
nianze kumlisha mtu nimpendaye. Nikamuanza mama, kisha nikamuita balozi
Brayan, pam