LIFE AFTER NOW

Learning about tommorow

Jumamosi, 30 Januari 2016

Eritrea yakerwa na habari ya wake wawili

Eritrea yakerwa na habari ya wake wawili

Januari 2016

Image copyrightBBC World ServiceImage captionWawili waliooana

Habari ya mzaha kwamba wanaume wa taifa la Eritrea wameagizwa kuoa wake wawili, ambayo imesambaa barani Afrika imewaudhi maafisa wa taifa hilo.

''Hata mwendawazimu katika mji mkuu wa Asmara atajua kwamba habari hii sio ya kweli'',afisa mmoja wa ubalozi wa Eritrea Kenya ameiambia BBC.

Habari hiyo ilichapishwa katika mtandao wa kitengo cha gazeti la The Standard la Kenya cha Crazy Monday.

Baadhi ya watu wametoa maoni yao katika mtandao wa Twitter kwamba wako tayari kusafiri hadi Eritrea ili kutafuta wanawake wa kuoa.

''Jarida la Crazy Monday ambalo huchapishwa na gazeti la Standard hujulikana sana kwa stori zake za udaku, likiwa ni mpango wa kutaka kuwavutia vijana," anasema Mathias Muindi wa BBC Media Monitoring.

Lakini hilo halijazuia taarifa hiyo kuripotiwa katika mataifa ya Nigeria hadi Afrika Kusini huku wengine wakisema kuwa ni ukweli.

Habari hiyo inasema kwamba ili kuhakikisha kuwa kuna wanaume walio wachache nchini humo wanaokidhi mahitaji ya wanawake walio wengi, kufuatia vita kati ya taifa hilo na Ethiopia mwaka 1998-2000, kila mwanamume lazima aowe wake wawili la sivyo afungwe jela.

Lakini afisa wa ubalozi wa Eritrea aliyezungumza na BBC amesema idadi ya wanawake na wanaume inakaribiana.

Waziri wa habari nchini Eritrea Yemane Gebremeskel alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter akisema kwamba habari hiyo ni ya uvumi, sio ya kweli na inakera.

WAZIRI WA AFYA NA HUDUMA ZA AFYA

#HABARI Naibu waziri wa Afya, Dkt Hamisi Kigwangala atoa mbinu za kuziwezesha hospitali za umma kuongeza mapato kwa kuboresha huduma kwa watu wenye pesa zaidi.
Ahoji :- "Kama matajiri hawaji kwenye hospitali za umma, mnategemea hawa maskini watapata pesa wapi za kulipia huduma?"

Taarifa kamili iko hapa;-
http://www.eatv.tv/news/current-affairs/kigwangala-ataka-mapato-zaidi-hosptali-za-umma

TANZANIA OPPORTUNITY


Umeisikia hii fursa kwa wale wanaopenda kuwa wafanyabishara wakubwa? CEO wa METL na Mwenyekiti wa Mo Dewji Foundation, Mohammed Dewji  wakishirikiana na Darecha anazungumzia shindano la Mo Entrepreneurs Competition walilolianda ili kukupa nafasi wewe. Tazama video ili uweze kushiriki na kujishindia hasa kwa wewe unayependa kuwa mfanyabiashara mkubwa hii inakuhusu sana.. SHARE na wengine pia wanufaike

https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=1422961194384961&id=157303284284098

AFRIKA ONE

Remember the 'white saviour' cameo in Africa in 90 seconds? Well this is #whatreallyhappened. Watch the full episode here: https://youtu.be/we53H9XZaas #tbt

#WHITEHOUSE

"Today, we’re taking one more step in the right direction. We are proposing to collect and report pay data by race, ethnicity, and gender from businesses with 100 employees or more. And the goal is to help businesses that are trying to do the right thing, like the ones here today, to get a clearer picture of how they can ensure their employees are being treated equally. A better picture of the data will also help us do a better job enforcing existing equal pay laws. " —President Obama announcing new actions to advance #EqualPay on the anniversary of the Lilly Ledbetter Fair Pay Act: go.wh.gov/EqualPay

FAHAMU KUHUSU MWEKEZAJI ALIYEKIMBIA NA KURUD KWAO INDIA

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwekezaji wa kiwanda cha kutengeneza nyuki Mkoani Tabora amefunga kiwanda hicho na kurudi makwao India.
Isome zaidi hapa http://www.eatv.tv/news/current-affairs/mwekezaji-afunga-kiwandaaondoka-na-funguo-india

NEWZ radio one newz

#Habari:Serikali imeuwasilisha na kuuondoa mpango wa pili wa maendeleo ya taifa kwa kipindi cha miaka mitano baada ya kubainia kuwa kuna kanuni na tararibu ambazo zimekiukwa katika kuwasilisha mpango huo bungen.->http://bit.ly/1TrMi5a

Jumatatu, 21 Desemba 2015

BUDDHIST MONKS LIVE

 NEWS 12 LIFE-CHANGING RULES BUDDHIST MONKS LIVE BY SPIRIT SCIENCE  What is your impression of the day-to-day of a Buddhist monk? Your visualization may make it appear that the monk-life is a vast departure from modern society, and you’d be pretty close to the truth. However, we can draw inspiration from the way they live their lives. If you are looking to bring more mindfulness and peace to your days, then we can look to these simple Zen Buddhist-inspired rules to live by, no matter what your spirituality or religion. One Thing At A Time. Take steps, rather than multi-tasking. For example: when eating, just eat. When bathing, just bathe. “When walking, walk. When eating, eat.” – Zen proverb. Slow and Steady Wins The Race Now that you’re doing one thing at a time, don’t rush it. Instead, take your time, move slowly, and act deliberately. Focusing like this is surprisingly difficult for someone used to rushing around doing a million things at once. Practice makes perfect, though. Follow Through. You’re doing one task slowly and deliberately, now make sure you follow through and finish it before moving on to the next. If it is impossible, at least try to put away and clean up the unfinished task so that it doesn’t interfere with your next movements. Do Less.

Alhamisi, 5 Novemba 2015

Faida za mende kwa maisha ya binadam kwa ujumla

Image copyrightThinkstockImage captionMende wana manufaa mengi sana kwa binadamu

Mende huchukiwa sana na watu na huhusishwa na uchafu na maradhi. Lakini wajua kwamba wadudu hawa wana manufaa makubwa sana kwa binadamu?

Mjini Havana, nchini Cuba kuna aina ya mende ambao hufugwa kama wanyama vipenzi na hata visa vyao husimuliwa kwenye hadithi, anasimulia Mary Colwell.

Kwenye kisa kimoja, mende kwa jina Martina huwafanyisha mtihani wanaotaka kumchumbia kwa kuwaudhi kila wanapomtembelea.

"Mwaga kahawa kwenye viatu vyao uone watalichukulia vipi hilo,” anapendekeza nyanyake Martina. "Ni muhimu sana kujua mumeo mtarajiwa hufanya nini anapokasirika – mtihani wa kahawa hufanikiwa.”

Kuna aina 4,500 ya mende, na ni aina nne pekee ambao huwa waharibifu.

Wengi hawaishi karibu na nyumba za watu na hutekeleza jukumu muhimu katika ikolojia kwa kula vitu vilivyokufa na vinavyooza.

Image captionBaadhi ya mende huishi pamoja na kusaidiana

Baadhi wana sifa nzuri na huishi pamoja na kusaidiana katika kutafuta chakula na makazi. Wana uwezo wa kuishi katika mazingira magumu. Aina moja kwa jina Eublaberus posticus wanaweza kuishi mwaka mmoja kwa kunywa maji pekee.

Wale wazito zaidi, huwa na uzani wa gramu 35, na urefu wa sentimeta 8 na huishi Australia. Wale wadogo zaidi huishi Ulaya na Amerika Kaskazini na wana urefu wa sentimeta moja pekee.

Badala ya kuwachukia, wanasayansi huwafurahia sana na kuwatumia kwa manufaa ya binadamu. Mwaka 1999, mende walitumiwa na Prof Robert Full katika Chuo Kikuu cha California, Berkley, kumpa wazo la kuunda roboti ya miguu sita iliyosonga upesi na kwa urahisi.

Mende huwa thabiti sana, na wakianguka huwa wanainuka upesi na kwa urahisi kwa kutumia mabawa.

Miguu ya mende pia imekuwa ikitumiwa na wavumbuzi wanaotengeneza miguu bandia ya kutumiwa na binadamu.

Kuna pia mende ambao wamekuwa wakiunganishwa na kompyuta ndogo inayowekwa mgongoni na kuongozwa kufika maeneo ambayo mwanadamu hawezi kufika.

"Nilipoona hili mara ya kwanza, nilishangaa sana,” mtafiti mkuu katika mradi huo unaoendeshwa katika Chuo Kikuu cha A&M cha Texas, Hong Liang anasema.

Mende wanatumiwa pia katika matibabu. Wanasayansi kwa miaka mingi wamekuwa wakishangazwa na uwezo wa mende kukaa muda mrefu maeneo yenye sumu na uchafu bila kudhurika. Wamegundua kwamba huwa wanatoa kemikali za kupigana na sumu.

Wanaweza kusaidia katika kutengeneza dawa za kusaidia binadamu kukabiliana na bakteria zinazohangaisha sana watu kwa mfano E. Coli na MRSA ambazo zimekuwa hazisikii dawa.

Hii si mara ya kwanza mende kutumiwa kwa sababu za kimatibabu. Mwanahabari Lafcadio Hearn karne ya 19 alipitia maeneo ya kusini mwa Marekani na kuripoti jinsi watu wenye pepopunda walivyokuwa wakipewa chai iliyotengenezwa kwa kutumia mende.

“Sijui ni mende wangapi hutumiwa hadi upate kikombe cha chai, lakini wakazi wa New Orleans wana imani sana na tiba hii,” aliandika.

Leo katika hospitali Uchina, krimu inayotengenezwa kwa kutumia ungaunga wa mende waliosiagwa hutumiwa kutibu vidonda vya moto na pia humezwa kutibu vidonda vya tumbo.

Mende wanahitajika sana hivi kwamba Wang Fuming aliamua kufungua biashara ya ufugaji mende eneo la Shandong, mashariki mwa Uchina. Huwa anafuga mende 22 milioni kwa wakati mmoja. Anasema tangu 2010, bei ya mende waliokaushwa imepanda mara kumi.

Jumamosi, 31 Oktoba 2015

TATHIMIN YA MCHEZO KAT YA CHELSEA NA LIVERPOOL

chi yamalizika Chelsea 1-3 Liverpool

Dakika ya 90+4: Mechi inamalizika. Mourinho anamsalimia Klopp na kuondoka uwanjani.

Dakika ya 90+2: Zouma anatuma krosi eneo la hatari lakini inapaa juu na kutoka nje.

Dakika ya 90+1: Adam Lallana anaondolewa uwanjani na nafasi yake anaingia Dejan Lovren

Dakika ya 90: Coutinho anashambulia tena. Anapata kona. Mpira unarejeshwa safu ya kati na kisha kwa kipa wa Liverpool.

Image copyrightAP

Dakika ya 82: BAOOOO! Christian Benteke!Chelsea 1-3 Liverpool.

Image copyrightGetty Images

"Utafutwa asubuhi" mashabiki wanaimba wakimkejeli Mourinho. Baadhi ya mashabiki wa Chelsea wanaanza kuondoka uwanjani. Wengine bado wanaimba jina lake.

Dakika ya 80: Chelsea wanashambuliwa tena. Nusura bao liingie.

Dakika ya 75: Alberto Moreno anapata nafasi na kushambulia. Kipa wa Chelsea Begovic anachomoka na kutupa nje kombora lake.

Dakika ya 73: BAOOOOOO! Coutinho! Chelsea 1-2 Liverpool.

Dakika ya 71: Cesc Fabregas anaingizwa nafasi ya John Obi Mikel, huku Chelsea wakiendelea kushambulia.

Dakika ya 70: Chelsea wanapata kona. Inachapwa na Willian lakini haizai matunda.

Dakika ya 68: Lucas Leiva ambaye tayari ana kadi ya njano anamchezea vibaya Ramires. Wachezaji wa Chelsea wanamzingira Mark Clattenburg. Lakini refa hachukui hatua yoyote. Anamuonya tu mchezaji huyo.

Dakika ya 63: Emre Can anapewa kadi ya njano.

Dakika ya 62: Nahodha wa Liverpool James Milner anaondolewa uwanjani na utepe wa unahodha unakabidhiwa Martin Skrtel.

Dakika ya 61: Kenedy nusura afanye mambo. Kenedy anatoa kombora kutoka hatua 18 lakini linaenda nje.

Ramires naye anapata nafasi nzuri lakini mpira wake unazuiwa na Martin Skrtel na Emre Can.

Dakika ya 59: Eden Hazard anatolewa uwanjani na nafasi yake anaingia Mbrazil Kenedy.

Dakika ya 57: Lucas anaonyeshwa kadi ya njano.

Dakika ya 49: Liverpool wanashambulia. Cahill anautoa mpira nje kwa kichwa na inakuwa kona. Tena Cahill anautoa nje wakati huu kwa mguu. Kona nyingine inapigwa lakini kombora la Coutinho linapaa na kupitia juu ya goli.

Dakika ya 49: Ramires anatoka nyuma na kumkabili Coutinho safu ya kati. Refa anatoa frikiki.

Dakika ya 47: Liverpool wanapata nafasi nzuri. Firmino ana mpira, lakini Zouma anaufikia na kuupiga nje.

Dakika ya 46: Chelsea wanashambulia. Lakini kombora la Willian linapinduliwa kisha kunyakwa na kipa.

Mechi inaanza kipindi cha pili.

Ni muda wa mapumziko sasa. Chelsea 1-1 Liverpool

Dakika ya 45+3: BAOOOO! Coutinho anasawazishia Liverpool. Chelsea 1- 1 Liverpool

Image copyrightReuters

Dakika ya 41: Diego Costa anakimbiza mpira eneo la Liverpool lakini unatoka nje kabla yake kuufikia.

Dakika ya 37: Mpira wa mbali unatumwa eneo la hatari la Chelsea. Lucas anaufikia kwa kichwa lakini mpira wake unanyakwa na kipa. Zouma analala chini akionekana kuumia lakini baadaye anainuka na kuendelea na mechi.

Dakika ya 35: Liverpool wanadai Terry amenawa mpira baada ya kutuliza krosi ya Nathani